NENO LA BWANA (KAWAA PARISH) 1. Neno la Bwana laleta uzima, neno la Bwana lakuja tulipokee. Neno la Bwana mwanga wetu sote - neno la Bwana lakuja tulipokee. K. Lapanda milimani,(neno) lashuka mabondeni (neno) Laenea pande zote neno lasonga mbele x2 2. Neno lapenya lafikia moyo - neno la Bwana latubadilisha mioyo. Tulipokee tutafaidika - neno la Bwana linao uzima tele. 3. Neno la Bwana ni nguzo kwa wote - walishikao daima watafurahi. Tutajulishwa Mungu asemavyo - tukiyashika sisi wana wake kweli. 4. Neno linao uzima kwa wote - halibangui wote wamekaribishwa. Twayashiriki mazuri ya mbingu - Mungu apenda wote walishike neno.
Where can we get the lyrics of the songs
NENO LA BWANA (KAWAA PARISH)
1. Neno la Bwana laleta uzima, neno la Bwana lakuja tulipokee. Neno la Bwana mwanga wetu sote - neno la Bwana lakuja tulipokee.
K. Lapanda milimani,(neno) lashuka mabondeni (neno)
Laenea pande zote neno lasonga mbele x2
2. Neno lapenya lafikia moyo - neno la Bwana latubadilisha mioyo. Tulipokee tutafaidika - neno la Bwana linao uzima tele.
3. Neno la Bwana ni nguzo kwa wote - walishikao daima watafurahi. Tutajulishwa Mungu asemavyo - tukiyashika sisi wana wake kweli.
4. Neno linao uzima kwa wote - halibangui wote wamekaribishwa.
Twayashiriki mazuri ya mbingu - Mungu apenda wote walishike neno.