EXCLUSIVE: HUYU NDIO PRODUCER MIKKA MWAMBA
HTML-код
- Опубликовано: 13 дек 2024
- Kama muziki unaoupenda ni Bongofleva na umekua ukiufatilia toka kitambo, jina la Mikka Mwamba halitakua geni kwako sababu ni Producer Hodari ambae mikono yake ilihusika kuzisuka Hits kama 'Barua' ya Daz Nundaz, 'Salome' ya Dully Sykes, Album ya kwanza ya Saida Karoli, Elimu mitaani ya D Knob na nyingine nyingi.
Ni wengi hawakua wanafahamu kwamba Mikka sio raia wa Tanzania au ni 'mtasha' na hiyo yote ni kwasababu aliamua toka kitambo asionekane kwenye Media wala kupigwa picha lakini leo amekubali kukaa kwenye ON AIR WITH MILLARD AYO.
Jina lake la kuzaliwa ni Mikka Kari ambapo hilo Kari kwa nyumbani kwao Finland linamaanisha 'mwamba wa baharini'