NENO LA SIKU | Luka 13 | Maombi Ya Kurudishiwa Nafasi Yako | Isaac Javan
HTML-код
- Опубликовано: 8 фев 2025
- Leo tunasoma kitabu cha Luka sura ya kumi na tatu, na tunaenda kufanya maombi ya kurudishiwa nafasi yako. Kuna watu wamepoteza nafasi zao katika familia. Wengine wamepoteza nafasi za kazi. Wengine wamepoteza nafasi kwenye ndoa zao. Wengine wamepoteza nafasi kwa watoto wao, na hawajui cha kufanya. Maombi haya yanakuja kwako yakiwa na lengo la kukusaidia urudishiwe nafasi yako iliyopotea.
Nakuombea upokee ushindi mkuu katika maombi ya leo. Eneo lolote ulilopoteza nafasi, Mungu akurudishie na akupe nafasi nyingine. BWANA akupiganie na kukushindia kwa utukufu wa jina lake. Ili kupata matokeo mazuri ya maombi haya, nakushauri uombe kwa kumaanisha, na utamuona Mungu akikupigania na kukutetea. Damu ya YESU inene maneno mazuri kwa ajili yako. Ameen!
Isaac Javan
+255 745 76 45 72