BUS LA SAULI LASABABISHA AJALI KIFO(1) NA MAJERUHI(1) RPC ATHIBITISHA...

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 20 сен 2024
  • AJALI YA BUS SAULI PWANI .
    Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani linamshikiria dereva wa Bus la Sauli Bw. TITO GADAU miaka 32 mbena na mkazi wa Mbezi Dar es Salaam kwa Chanzo cha ajali kwa kulipita gari lililokuwa limesimama na matokeo yake akagongana na pikipiki iliyokuwa inakuja mbele yake Sambamba na tukio hili Jeshi la Polisi linawashikiria watu wapatao nane (08) kwa tuhuma za kulishambulia Bus lililosababisha ajali na kulivunja vunja vioo kwa kutumia mawe.
    Mnamo tarehe 16/11/2021 majira ya saa 01:00 jioni katika eneo la Kwa Mathias kata ya Mkuza wilaya ya Kibaha kwenye barabara kuu ya Morogoro, gari la abiria Kampuni ya SAULI Na. T 668 DCF Scania ikitokea Mbeya kwenda Dsm likiendeshwa na Bw. TITO GADAU miaka 32 mbena mkristo mkazi wa Mbezi Dar es Salaam, iligonga pikipiki (bodaboda) MC 606 CAQ Sanlg iliyokuwa inaendeshwa na EDWIN RODRICK MWENDA miaka 25 mkazi wa Kwa Mathias akiwa amembeba abiria aitwaye EMMA NAMBOLE miaka 37 mkazi wa Kibondeni Kwa Mathia imesababisha kifo cha abiria wa pikipiki na majeruhi kwa dereva wa pikipiki EDWIN RODRICK MWENDA.
    INSERT.WANKYO NYIGESA -Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani.
    Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Tumbi ili kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu. Dereva wa pikipiki (majeruhi) Bw. EDWIN RODRICK amelazwa katika hospitali ya Rufaa Tumbi.
    Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa bus kulipita gari lililokuwa limesimama na matokeo yake akagongana na pikipiki iliyokuwa inakuja mbele yake.
    Sambamba na tukio hili Jeshi la Polisi linawashikiria watu wengine wapatao nane (08) kwa tuhuma za kulishambulia Bus lililosababisha ajali na kulivunja vunja vioo kwa kutumia mawe.
    Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani linakemea vikali tabia ya wananchi wachache kujichukulia sheria mkononi kwa kisingizio cha hasira kali kama ilivyotokea katika tukio hili. Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani halitavumilia mihemko ya watu wachache wasiopenda kutii sheria. Tunakusudia kufanya operesheni kali ili kuwakamata wote waliohusika kuharibu na kurusha mawe ambayo pia yalimjeruhi askari Polisi wa Usalama Barabarani aliyekuwa eneo hilo akifanya kazi za kuongoza magari. Askari huyo F.3490 SGT OKOKA CLAUS MBAFU amelazwa hospitali ya Tumbi baada ya kushambuliwa kwa mawe alipofika eneo la tukio kwa ajili ya kuchukua hatua.
    INSERT.WANKYO NYIGESA -Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani.
    ..….MWISHO…….

Комментарии • 1