TADB na JICA 2025
HTML-код
- Опубликовано: 5 фев 2025
- Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Fedha, imesaini mikataba miwili ya muhimu ambapo mkataba mmoja ni kwaajili ya Wizara ya Fedha pamoja na Ubalozi wa Japan wa pili ni mkataba wa mkopo kati ya Wizara ya Fedha na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA)
Kusainiwa kwa nyaraka hizi kunawezesha serikali ya Japan kuipatia Serikali ya Tanzania mkopo nafuu wa Yen za Kimarekani Milioni 22.72 sawa na Shilingi Bilioni 354.45 kwaajili ya utekelezaji wa miradi wa uendelezaji wa kilimo vijijini unaojulikana kama "The Agricultural and Rural Development Two step Loan Project"
Ufadhili huu utasimamiwa na JICA kwa niaba ya Serikali ya Japan kupitia mkataba wa mkopo huu na kwa upande wa Serikali ya Tanzania mradi huu utatekelezwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania @tadbtz