Sheikh Nassoro - Bachu Mauti B
HTML-код
- Опубликовано: 7 фев 2025
- Kila nafsi itaonja mauti.
Ni glasi inayozunguka kwa kila mtu, awe mwema au muovu mfalme au kabwela. Haiwezekani wala hakuna njia yoyote ya kuyakimbia mauti. Lile wanalofikiria madaktari ni kujaribu kurefusha maisha ya mtu tu, sio kukinga mauti.
Jaribio la mwisho walilifanya madaktari la kurefusha maisha mwaka 1967, ni kupachika moyo mwengine wa mtu anayekaribia kufa, anatolewa moyo na kuwekwa kwa mwenye moyo mgonjwa baada ya kutolewa.
#SheikhNassoroBachuMauti #bachumauti #mawaidhayamauti #mautiuislamu #pindibindamuanapokufa #SheikhNassoro
Lakini jaribio hili halikufanikiwa, ingawaje lilifanyika mara kwa mara. Kukawa na mzozo kwa madaktari wakubwa wakasema hilo ni kosa lisilosameheka. Kwa sababu haiwezekani kuhakikisha kuwa yule anayetolewa moyo kweli angekufa baada ya muda mfupi? Kwani kifo hutokea kwa namna tofauti; kama vile kuzimia muda mrefu na kukosa kuvuta pumzi, wala hakuna njia ya kujua hali hii baina ya kifo na uhai. Mara ngapi madaktari wamethibitisha kifo, kisha wagonjwa wakarudiwa na uhai.
Jana nimesoma katika gazeti moja kwamba kikongwe mmoja Mmisri alizimia, watoto wake wakaita madaktari, wakathibitisha bila ya wasiwasi kwamba amekufa, baada ya kutangaza kifo, kutoa matangazo ya tanzia, kuchimba kaburi na watu kuhudhuria mazishi, alifungua macho yake na akawaambia watu waliokuja: "Nendeni kwenye shughuli zenu Mungu awalipe."
Ikiwa madaktari wameshindwa kuurefusha umri wa mtu na hata kumjua kama amekufa au ni mzima, basi kumkinga na mauti ndio hawawezi kabisa.