Zuchu Ft. D Voice - Hujanizidi (Lyrics)
HTML-код
- Опубликовано: 14 янв 2025
- Hujanizidi lyrics by Zuchu ft D Voice
Stream/Download
Yaani mara kumi ungekuwa mbaya, halafu ungekuwa na hela
Lakini tatizo lako mbaya halafu hauna hela
Ni mara kumi ungekuwa kijuso, halafu ungekuwa na hela
Ila tatizo lako kijuso halafu hauna hela
Ah, sa' mbona unapata tabu kujichubua
Tako huna unaforce kujibinua
Baby wangu hajadata na chura ka' hujajua
Kadata na mambo matamu ninayomgea, nikwambie wewe
Kwa uzuri hujanizidi mimi
Kwa utamu hujanizidi shoga yangu
Kwa uzuri hujanzidi mimi
Kwa utamu hujanzidi shoga yangu
Na huyo baby wako alikuwa wa kwangu
Kabla ya kuwa wa kwako
Hauniambii kitu kuhusu yeye
Hata kulala, alilala kwangu, kabla ya kulala kwako
Kwahiyo hunitishi mbwa wewe
Oya weh, hakuna ulichonizidi cha kunipa stress
We nyota yako ya kuni, mie mwenzako ya gesi
Mwenzako uzuri wangu natural sio wake wa kufeki
Maana mwenzangu una rangi nyingi ka' combati ya jeshi
'Asa mbona unapata tabu kujichubua
Tako huna unaforce kujibinua
Baby wangu hajadata na chura ka' hujajua
Kadata na mambo matamu 'nayomgea, nikwambie wewe
Kwa uzuri hujanizidi mimi
Kwa utamu hujanizidi shoga yangu
Ooh! Kwa uzuri hujanizidi mimi
Ai udugu we kwa utamu hujanzidi shoga yangu
Haunitishi hunisumbua (hujanizidi
mimi)
Jiangalie kuvaa hujui (hujanizidi shoga
yangu)
Ay! Hapo kwanza nicheke, haaa!
Wanangu bado sijaskia shangwe kama umeme umerudi (huoo!)
Masela bado sijaskia shangwe kama umeme umerudi (huoo!)
Ay! Mara tena umekata (aah!)
Mama, mara tena umerudi (huoo!)
Wewe, mara tena umekata (aah!)
Twende, show me gidi, gidi, gidi
Baby gidi, gidi, gidi
Twende gidi-gidi-gidi, gidi we
Gidi, gidi, gidi
Kwanza muone amepandwa na ibilisi
Alikaa pembeni, hivi sasa ameingia kati
Ona mwili mkubwa kumbe kibonge mwepesi
Kulia kushoto, dunda kama kitenesi
Twende sasa gidi, gidi, gidi
Gidi, gidi, gidi
Twende gidi-gidi-gidi, gidi
Gidi, gidi, gidi
Hapo kwanza nicheke, hahaaa!
Oya we! we hili goma noma kwani amelipiga nani
Maana inafanya wanangu mpaka wanapandwa shetani
We hili goma noma kwani amelipiga nani
Maana wanavua mashati kwenye miti wanachuma majani
Oya wanachuma majani, Wanaleta majani mama
Wanachuma majani, Wanaleta majani oya
Diblo nipe, nipe tena, Diblo nipe (DJ Kidogodogo) nipe tena
Tags;
Zuchu new song
Hujanizidi by Zuchu ft D Voice Zuch ft D Voice Hujanizidi lyrics
Zuchu ft D Voice
Hujanizidi lyrics by Zuchu ft D Voice Wasafi records
#Zuchu #Hujanizidi #PeaceandMoney #music #lyrics #wasafi #Dvoicel
Je, note mna maoni gani kuhusu wimbo huo? Shiriki mawazo yako hapa chini.💬
Nimengojea hii Ngoma tokea wamemsign Dvoice🎉🔥🔥🔥
Singeri za aina hili ndo zinakuaga Tamu Apa namkumbuka D voice yule wa zaman daah
Nice lyrics 😊
I knew this would be a hit 🔥
🔥🔥