WITO WA KUUJUA WAKATI SEH: IV
HTML-код
- Опубликовано: 7 янв 2025
- Neno la Mungu katika 1Nyakati 12:32 linasema hivi; "Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao". Swali ni hili, je, siku hizi za mwisho hatuhitaji kuwa na akili za kuzijua nyakati tunazoishi ili kwa kujua huko kutusaidie kujua nini tunapaswa kutenda? Jibu ni kwamba akili za kuzijua nyakati tunazihitaji hata sasa. Kwa sababu hiyo basi, somo hili "WITO WA KUUJUA WAKATI SEH: IV" linakujia wakati ambapo nyakati tunazoishi zinatuonesha ya kwamba tumeufikia ule mwisho na Yesu yupo karibu sana kuja mara ya pili. Kwa hiyo, ukweli kuhusu matukio ya siku za mwisho unahitajika sana. Katika somo hili ukweli huo umewasilishwa, hivyo, utapata kujifunza mengi yatakayokufanya uelewe wapi tumefika katika historia ya kinabii na tunapaswa kufanya nini?. Somo hili katika video hii ni matokeo ya kuitikia WITO WA BWANA unaotutaka walinzi kupaza sauti, nabii Ellen G. White anasema hivi; “Wakati ulimwengu wa Kiprotestanti kwa mtazamo wake unafanya makubaliano na Rumi, hebu tuamke na kuelewa hali na kuona mashindano yaliyo mbele yetu katika uhalisia wake. Hebu walinzi sasa wapaze sauti zao na kutoa ujumbe ambao ni ukweli wa wakati huu. Hebu tuwaonyeshe watu wapi tumefika katika historia ya kinabii na tutafute kuamsha roho ya Uprotestanti wa kweli……...” {5T 716.2}. Kwa kweli uprotestanti umeshafanya makubaliano na Rumi na hivi karibuni sheria ya jumapili itapitishwa nchini Marekani, kwa hiyo, huu ndio wakati wenyewe hasa wa kujua yatupasayo. Endelea kufuatilia masomo haya, share na wengine, usisahau ku-subscribe ili upate somo jipya kila siku ifikikapo saa kumi na mbili kamili jioni.
Nabarikiwa sana
Ubarikiwe mno Pr kazi yako njema Mungu anaiona
@@grecemakalwe8286 Jina la Yesu litukuzwe sana, atufunuliaye haya na kutupa ujasiri na nguvu za kuutangaza ukweli
Salaam ktk Kristo Yesu, karibuni kwa maswali, usisahu ku-subscribe ili upokee masomo zaidi kila siku
Mchungaji ubarikiwe kutufunulia haya mm niko geita nnakufatiria sana kila somo unalotoa
@@JamesiSamweli-h3f Jina la Yesu litukuzwe sana kwa mafunuo ya ukweli wake, barikiwa na Bwana
Mchungaji mm huku nabarikiwa
@@Musakib-j1d Jina la Yesu litukuzwe sana, endelea kubarikiwa na Bwana