Safari ya Mkimbizi ya Kupata Makazi Mapya Nchini Kanada

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 4 окт 2024
  • Video hii ilirekodiwa kabla ya kutokea kwa janga la COVID-19. Huenda baadhi ya picha hazionyeshi hatua za sasa za kudumisha umbali wa kutokaribiana na mtu mwingine.
    Hali ya kupata makazi mapya nchini Canada kama mkimbizi inaweza kuwa yenye changamoto, matumaini na matarajio mengi.
    Ni muhimu kujua unachotarajia na huduma na usaidizi unaopatikana kwa ajili yako kama mkimbizi aliyepata makazi mapya ili kukusaidia kuishi nchini Canada.
    Kabla ya kuwasili, unaweza kupata mafunzo kuhusu Maelekezo ya Mazingira ya Kanada Ukiwa Nje ya Nchi kutoka kwa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji. Mafunzo haya yatakusaidia upate maelezo zaidi kuhusu Canada na jinsi ya kujiandaa kwa safari.
    Unapowasili nchini Canada kwa mara ya kwanza kama mkimbizi aliyepata makazi mapya, shirika linalofadhiliwa na Serikali ya Kanada au wafadhili wako binafsi watakusaidia kukidhi mahitaji yako ya dharura. Watakukaribisha utakaposhuka kwenye ndege, watakupa mahali pa kukaa kwa muda na kukusaidia upate makazi ya kudumu. Watakusaidia pia ufungue akaunti ya benki, kuhakikisha kuwa watoto wako wamepata shule na kujifunza jinsi ya kuishi katika jamii yako mpya.
    Kama mkimbizi aliyepata makazi mapya nchini Canada, unaweza pia kupata huduma za makazi zisizolipishwa ili kukusaidia uzoee na ufaulu kuishi katika jamii yako mpya.
    Huduma hizi hutolewa na mashirika yanayofadhiliwa na Mpango wa Makazi wa Serikali ya Kanada na zinaweza kukusaidia:
    • Utengeneze mpango wa makazi unaokufaa zaidi kulingana na uwezo na mahitaji yako na uelekezaji kwa vikundi au mashirika ambayo yanaweza kukusaidia.
    • Upate maelezo zaidi kuhusu maisha nchini Kanada.
    • Ujifunze lugha ya Kiingereza au Kifaransa.
    • Upate kazi, ukuze mtandao wako wa kitaalamu na uendeleze taaluma yako.
    • Uungane na wenyeji na wageni wengine katika jamii yako.
    Ili upate huduma za makazi zisizolipishwa zilizo karibu nawe, tafadhali tembelea: www.cic.gc.ca/...
    Pata majibu ya maswali yako kwenye mitandao ya kijamii:
    Facebook: Uraia na Uhamiaji Nchini Kanada / citcanada
    Twitter : @CitImmCanada
    / citimmcanada

Комментарии •