Mafunzo ya Utengenezaji Simu za Mkononi yanayotolewa katika Chuo cha VETA Kipawa

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 8 сен 2024
  • Kipindi cha Ujuzi ni Maisha Mafunzo ya Utengenezaji Simu za Mkononi yanayotolewa katika Chuo cha VETA Kipawa
    Kulingana na takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania-TCRA za mwaka jana 2019, kuna laini za simu za mkononi zipatazo milioni 40. Kwa upande mwingine, Taarifa ya Uchumi wa Simu za Mkononi iliyozinduliwa nchini mwaka jana, inaonyesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa manane barani Afrika ambayo yana soko kubwa la simu za mkononi.
    Ni dhahiri kuwa matumizi ya simu za mkononi ambayo yanazidi kuongezeka kila siku yanaleta mchango mkubwa sana katika maendeleo na kurahisisha maisha ya watu wengi.
    Kukua na kupanuka kwa matumizi ya simu za mkononi kunazaa hitaji kubwa la mafundi wa simu hizo, kwani kama ilivyo kwa vifaa vingine, simu hizo nazo huaribika na kuhitaji matengenezo au marekebisho.
    Uhitaji wa matengenezo ya simu hizo umeibua fursa ya ajira kwa vijana wengi nchini wanaojulikana kama mafundi simu ambao wamekuwa wakijipatia kipato na kuendesha maisha yao kutokana na kazi hiyo.
    Hata hivyo, kumekuwa na changamoto kubwa ya uwepo wa mafundi simu wasiokuwa na ujuzi wa kufanya kazi hii, hali inayosababisha malalamiko mengi kutoka kwa watumiaji. Vijana wasiokuwa na ujuzi mara nyingi hufanya uharibifu zaidi kwenye simu wanazopewa kufanyia matengenezo na kusababisha hasara kwa wateja wao.
    Kwa kutambua changamoto hiyo TCRA imeingia makubaliano na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kushirikiana katika kuimarisha ujuzi wa ufundi wa simu za mkononi ili kuwa na mafundi mahiri na wa kuaminika.

Комментарии • 12

  • @ShabanhasanShabanHasan-yc1gd
    @ShabanhasanShabanHasan-yc1gd 11 месяцев назад

    Kama kweli mmedhamiria basi hayamasomo yafanyeni mtandaoni ndio mtafikia watu wengi

  • @allykhamis155
    @allykhamis155 4 года назад +1

    Mbona Mimi natafuta appy hiyo sioni naomba nielekezwe maana natamani kupata mafunzo zaidi nikipata elimu naeeza kiwa mtaalam zaidi

  • @bigmark2857
    @bigmark2857 4 года назад

    good

  • @rangiwizzy3813
    @rangiwizzy3813 Год назад

    Muda wa mafunzo na sifa tafadhali

  • @jafarisaidi3926
    @jafarisaidi3926 Год назад

    Mimi naitaji huu ufundi nawezaje kusoma???

  • @jafarisaidi3926
    @jafarisaidi3926 Год назад

    Nahitaji kujifunza mimi

  • @user-jt6it7ij7h
    @user-jt6it7ij7h 11 месяцев назад

    nataka namba zenu

  • @vicentegeraldo433
    @vicentegeraldo433 3 года назад

    Number za offici ya Chuo nitapata wapi?

  • @ezirapetro8733
    @ezirapetro8733 4 года назад

    Hicho cho kipo wapi naomben mnijulishe