MEYA WA JIJI LA MBEYA ACHARUKA WAONDOENI WANAOKWAMISHA MRADI WA TACTIC

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 22 май 2024
  • Halmashauri ya Jiji la Mbeya imezitaka kampuni ya ujenzi ya Cico inayojenga jengo na barabara za mradi wa Tactic na Kampuni ya Mhandisi ambayo ni mkandarasi mshauri kwenye miradi hiyo kuwaondoa wasimamizi wake kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
    Akizungumza baada ya ziara ya kukagua ujenzi wa barabara za Kalobe-Itende, Machinjioni- Mapelele, Kabwe-Sido na Iziwa, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mhe.Dormohamed Issa amesema, hajaridhishwa na anapata wasiwasi na kasi ya maendeleo ya mradi na hana uhakika kama mkandarasi atamaliza mradi kwa wakati uliopangwa kwa mujibu wa mkataba.
    Mstahiki Meya ameongeza kuwa tangu mkandarasi wa kampuni ya Cico alipokabidhiwa na kuanza kazi Novemba, 2023 hakuna alichokifanya kwenye barabara zote, hali ambayo inasababisha wananchi kuendelea kukabiliwa na changamoto ya barabara wakati Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, imeshatoa fedha, hivyo amemtaka mkandarasi kumuondoa Meneja Mradi Mhandisi Bw.Penfeng Wang na Kampuni ya Mhandisi ambayo ni Mkandarasi Mshauri, Bw.Jofrey Kanjanja kwa kushindwa kusimamia kasi ya mradi kama ilivyopangwa.

Комментарии • 6

  • @davidlinus6940
    @davidlinus6940 Месяц назад +1

    Barabara mnasanifu bila kuweka njia za watembea Kwa miguu wasomi vp

  • @ayoubbalama1409
    @ayoubbalama1409 Месяц назад +1

    Wanacho jua nikufunga balabala na sio kazi wana zingua sana.

  • @juliabwana2519
    @juliabwana2519 Месяц назад +1

    Muikumbuke na barabara ya iyela makaburini wakazi wa kigamboni tunapata tabu sana muheshimiwa alituahidi lakini tunaona kimya sana

  • @user-ov7ge3ci6f
    @user-ov7ge3ci6f Месяц назад +1

    Apa Sasa Jiji ltkuwa ila sio mnvokaa tu ofsn
    Saf sna

  • @oscarwasenga1333
    @oscarwasenga1333 Месяц назад

    Nyie mmekata mipila barabara yamapele maji hayatoki mpk leo mnakuwa namaneno mengi TU bila vitendo

  • @tonyaron1194
    @tonyaron1194 Месяц назад

    Hapo meya hayupo unaongea kwa kulalamika badala ya kutoa onyo Kali ama kumfukuza kabisa huyo mkandalasi uki lalamika hivyo sisi wananchi tusemeje? Eti sehem zingine wanaenda vizuri, Wenzenu wapo serious na kaz na Wana uchungu na jiji lao lkn siyo nyie mnabembeleza watu