OTHMAN MAALIM - KISA CHA MFALME NAJASH WA ETHIOPIA/HABASH SEHEM YA PILI

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 7 фев 2025
  • OTHMAN MAALIM - KISA CHA MFALME NAJASH WA ETHIOPIA/HABASH SEHEM YA PILI
    Kwa wale wanaofuatilia matukio ya historia ya Uislamu, mfalme huyu ndiye aliyewakaribisha Waislamu wa mwanzo waliokimbia mateso makali ya waabudu masanamu wa Makka.
    Aliwakaribisha na kuwapa hifadhi na hata alipojiwa na makafiri na kumlaghai kwa rushwa na hongo, hakukubali kuwakabidhi wakimbizi hao kwa watesaji hao wa Makka.
    Katika mwaka wa saba wa Hijra, kufuatia Mkataba wa Amani wa Hudaybiyyah, Mtukufu Mtume (s.a.w), mtume aliyetumwa kwa watu wote, alianza kuyalingania mataifa ya karibu na yale ya mbali kuingia katika Uislamu.
    Amr ibn Umayyah (r.a) ndiye aliyewasilisha barua ya Mtume (s.a.w) kwa mfalme Najjashi wa Abyssinia (Ethiopia ya sasa).
    Mfalme Najjashi wa Abyssinia alionesha ukarimu wa hali ya juu kabisa kwa kuipokea barua ya Mtukufu Mtume (s.a.w) na kwa mjumbe aliyeiwasilisha, Amr ibn Umayyah (r.a).
    Pamoja na wito na ujumbe wa wazi wa kumlingania kwenye Uislamu, barua iliyotumwa kwa Najjashi pia ilikuwa na taarifa na maelezo mafupi kuhusu Bibi Maryamu na Nabii Isa (a.s).
    Akiwa ameshajifunza Uislamu kwa kiasi fulani kutoka kwa Waislamu ambao awali walihamia Abyssinia na akiwa amechukua hatua ya ujasiri ya kuupokea tokea mwanzo, Najjashi aliishikilia ndege ielekeayo kwenye anga ya imani baada ya kupokea barua rasmi ya kumuita kwenye Uislamu.
    Alitangaza imani yake mbele ya Ja’far (r.a), mtoto mkubwa wa Abu Talib, ambaye wakati huo alikuwa pamoja naye. Kisha katika kutekeleza maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w), aliwapakia kwenye majahazi mawili wahamiaji wa Kiislamu na kuwavusha upande wa pili wa Bahari Nyekundu.
    Vilevile alimtumia Mtukufu Mtume (s.a.w) barua yake mwenyewe, akieleza wazi kuwa ameshaingia katika Uislamu.
    Ilisema:
    “Kwa Muhammad (s.a.w), Mtume wa Mwenyezi Mungu, kutoka kwa Najjashi,
    Amani, rehma na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yako, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mwenyezi Mungu, ambaye hakuna mungu ila Yeye, ameniongoza kwenye Uislamu.
    Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu...! Nimepokea barua yako ambayo ndani yake umeelezea hali ya Isa (a.s). Naapa kwa Mola wa Mbingu na Ardhi, hakika ulichosema kumhusu ndicho hicho hicho alichokisema yeye. Ujumbe wake ulikuwa kama usemavyo. Tumejifunza misingi ya Uislamu ambao umepewa kazi ya kuutangaza. Tumempa hifadhi binamu yako (Jafar) pamoja na wenzake waliohamia katika ardhi yetu.
    Ninashuhudia kwamba wewe ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Maneno yako ni ya kweli. Wewe ni mkweli na mwenye kusadikishwa.
    Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Nimekula kiapo cha utii kwako kupitia kwa binamu yako, mwakilishi wako. Nimejisalimisha kwa Mola wa Ulimwengu mbele yake. Ninamtuma kwako mwanangu Arha.
    Sina mamlaka juu ya chochote zaidi ya nafsi yangu; na iwapo utataka nije kwako, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nitafanya hivyo mara moja. Ninashuhudia kwamba unachosema ni kweli.
    Amani iwe juu yako, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu...” (Ibn Sad, I, 259; Ibn Qayyim, III, 689; Hamidullah, al-Wasaiq, p. 100, 104-105)
    Nilipomaliza kuisoma hii barua ya Najjashi nilijikuta nikitokwa na machozi! Namuomba Allah atupe moyo thabiti kama wa Najjashi!
    #OTHMANMAALIMKISACHAMFALMENAJASHWAETHIOPIAHABASHSEHEMYAKWANZA #OTHMANMAALIMKISACHAMFALMENAJASHWAHABASH #KISACHAMFALMENAJASH #MFALMENAJASHI

Комментарии • 4

  • @MuslimuTv
    @MuslimuTv  2 года назад

    OTHMAN MAALIM - KISA CHA MFALME NAJASH WA ETHIOPIA/HABASH SEHEM YA KWANZA
    👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
    ruclips.net/video/I0Vxk5RxnFY/видео.html

  • @ummysaabersaeedy8152
    @ummysaabersaeedy8152 9 месяцев назад

    Kisa kizur sana Masha Allah

  • @ummysaabersaeedy8152
    @ummysaabersaeedy8152 9 месяцев назад

    Sauti kama sio ya othman maalim

  • @ashrunaomar9577
    @ashrunaomar9577 Год назад

    Mashaallah