Salama Na ROSE MUHANDO SE6 EP53 | NIPE UVUMILIVU PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 5 фев 2023
  • #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
    Katika binadamu ambao walinipa wakati mgumu na kusubiri kwingi kabla ya kuja kukaa kwenye meza yetu ya kigae na kiti chakavu basi mmoja wao ni Rose huyu wa Muhando. Upatikanaji wake ni kama ukitaka kumuona SIMBA mbugani, lazima uamke asubuhi na mapema au uwe na bahati ya mtende kama ambayo sisi tumepata. Ingawa tulisubiri kwa masiku tele na miezi tele katikati ya mwaka huu tuliweza kumpata na kukaa nae chini ili tuweze kuzungumza nae.
    Rose ni wa moto sana, kalenda yake imejaa safari tele za nje na ndani ya nchi, anazunguka mara kwa mara kwaajili ya kutoa elimu na burudani kwa watu wengi ambao nao pia wamekua wakimgojea kwa hamu na kwa masiku tele. Kipaji chake cha kipekee ndicho ambacho kimemfanya awe maalum miungoni mwa wasanii wanaofanya muziki wa Injili na uzuri wake mwengine ni kwamba amekua akitoa huduma hiyo kwa miaka mingi bila ya ‘kuchuja’.
    Sasa nini hasa siri ya mafanikio hayo?! Ukiachana na panda shuka tele ambazo Rose amepitia toka akiwa na umri wa miaka 6, kukata tamaa ni jambo ambalo halipo kabisa katika mambo ambayo huwa anayawaza. Pengine kujiuliza kwanini na anatokaje kwenye hilo zito alilo nalo linaweza likawa ndo swali, ila kusema kwamba hatoweza au haiwezekani hilo jambo kwenye kitabu chake au kichwani chake huwa halipo kabisa.
    Ukiskiliza kwa makini maneno ambayo yanatoka katika mdomo wake utagundua Rose ni mmoja kati ya wanawake jasiri sana ambao wamewahi kutokea katika kiwanda hiki cha Sanaa hapa Tanzania. Ukimuangalia macho yake, mikono yake ambayo imejaa makovu na nna uhakika pia kuna sehemu nyengine kwenye mwili wake pia zimejaa makovu lakini hatukuweza kuona unaweza ukapata tu idea ya makubwa na mazito ambayo amepitia na ambayo yameacha makovu makubwa tu si mwilini mwake tu bali hata kwenye moyo wake. Ananihadithia kwenye episode hii jinsi ambavyo watu walikua wanamuadhibu ki mwili na ki akili ikiwa ni pamoja na kupigwa, kuchomwa moto, kukatwa na kunyang’anywa mali zote ambazo amewahi kutengeneza tokea wakati anaanza muziki ila hayo yote hayajawahi kumkatisha tamaa wala kumrudisha nyuma.
    Rose anaamini na aliamini kwamba ana uwezo wa kuvipata vyote ambavyo watu walimdhulumu kwenye kipindi flani kwenye maisha yake, aliamini hakuna ambaye anaweza kumnyang’anya kipaji ambacho Mwenyezi Mungu amempatia na kwa kupitia hiko kipaji na akiwa hai na mzima basi vyote ambavyo aliwahi kuwa navyo na vikapotea basi alikua na uwezo wa kuvirudisha na ni kweli, kuvirudisha ameweza na vimekuja maradufu yake.
    Simulizi zake za safari yake toka siku ya kwanza alipokua mdogo nyumbani kwa Baba na Mama yake huko kwao Morogoro wakati anaumwa ni moja ya vitu vya kufikirisha sana ambavyo nimewahi kuvisikia toka tumeanza kukalia kiti chakavu, na yangu matumaini maongezi haya kwa kiasi kikubwa yatakupa ile vibe ambayo huwa naizungumzia kwenye intro ya kipindi chetu hiki.
    Tafadhali enjoy.
    Love,
    Salama.
    Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
    SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
    Listen our Podcast on
    Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
    ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
    GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
    Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
    ‪RUclips Link bit.ly/RUclipsSalamaNa
    Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
    Follow:
    Twitter: / yahstonetown
    Instagram: / yahstonetown
    Facebook: / yahstonetown
    Channel Administered by Slide Digital
    Instagram: slidedigitaltz
  • РазвлеченияРазвлечения

Комментарии • 191

  • @theafricaiknow6615
    @theafricaiknow6615 Год назад +17

    Kwa kweli kutokewa na Yesu katika umri mdogo mtoto hawezi kudanganya. Ni kweli alitokewa

  • @HabilyTech
    @HabilyTech Год назад +4

    HUU NI USHUHUDA YA KWAMBA YESU KRISTO MTOA UZIMA ANAISHI HALELUYAAAAA.

  • @gosbertgideon6843
    @gosbertgideon6843 Год назад +10

    Rose muhando muimbaji injili nimpendaye kutoka moyoni
    Snaga shaka nawww

  • @gb-one6435
    @gb-one6435 Год назад +18

    Miujiza kama hii ipo jamn sio uongo me pia yalisha nitokea maono makubwa ilibakia kidogo niangamie Mungu aka niinua Tena 🙏

    • @felixbenos6365
      @felixbenos6365 Год назад +1

      Pole sana mm pia nimepitia magumu sana ilikuwa nife bt Mungu akanipigania..ukweli Miujiza niliona nihatare

  • @officialjemimahowiti
    @officialjemimahowiti Год назад +9

    Your maturity questions are amazing, it makes your show be watchable by everyone

  • @LuckyBoy-pp2md
    @LuckyBoy-pp2md Год назад +11

    Mbona mnaumia jamaniiii kwakweli umenibaliki mama roseeeeeeeeeeee watazidi kuumia hao wasiemjua yesu jesus 4life

  • @salamanauthar5261
    @salamanauthar5261 Год назад +5

    Salama kapatikana walahi' hana hata la kuongea kabaki mdogooooo 🤣🤣🤣🤣🤣🤣

  • @naomimuthui6998
    @naomimuthui6998 Год назад +5

    May God bless you Rose and protect you as you continue preaching through singing

  • @G.S985
    @G.S985 Год назад +3

    Mungu ni mwema,Dada Rose uwagasichoki ushuhuda wake,ama kweli Mungu akikutaka huna kwa kukimbilia.

  • @pendokissatu937
    @pendokissatu937 Год назад +5

    QUEEEEN OF ALL THE TIME ❤️❤️❤️❤️❤️

  • @davisminja3742
    @davisminja3742 Год назад +3

    Mungu ni Mkuu siku zote hongera kwa Baba yako alisema kitu cha kweli hawezi ongea uongo akati aliona na atakuwa na pepo yakeee

  • @deneagrofarms5884
    @deneagrofarms5884 Год назад +3

    Hongera bibie SHADYA. MUNGU amekuchagua umtumie kwa iishara ya wazi kabisa isiyo na ukakasi

  • @princessshirima6664
    @princessshirima6664 Год назад +4

    Mungu alisimama na rose na hadi leo Anasimama naye bado mkon wa Mungu u juu yake

  • @stevennyondo2215
    @stevennyondo2215 Год назад +4

    Ushuhuda mzur ila MUDA mdogo , waiting for part two

  • @chikitongwaru7035
    @chikitongwaru7035 Год назад +2

    Yesu alikuokoa na umeupiga mwingi

  • @emmyjuma2987
    @emmyjuma2987 Год назад +1

    Mm nakuelewa

  • @darcasgodfrey8082
    @darcasgodfrey8082 5 месяцев назад +1

    HAKIKA YESU KRISTO NI BWANA 🙌

  • @mwaminiesperance6276
    @mwaminiesperance6276 Год назад +6

    You are a special person Rose may God continue to protect you ma ❤️ 🙏 ♥️ 💛

  • @francesmpangwa8801
    @francesmpangwa8801 Год назад +1

    Nakupenda sana Queen of gospel Rose Muhando

  • @G.S985
    @G.S985 Год назад +2

    Nakupenda bure Dada Rose

  • @christopheritambo1315
    @christopheritambo1315 Год назад +1

    One of my favorite artist her Majesty Rose Muhando

  • @farajakivuyo9389
    @farajakivuyo9389 Год назад +5

    The Best session on RUclips

  • @saidahj2543
    @saidahj2543 Год назад +2

    Rose you are my STRENGTH

  • @sophyeliah954
    @sophyeliah954 Год назад +2

    Here a Queen💌❤️

  • @Clivanny
    @Clivanny Год назад +1

    My mama🔥🔥

  • @brendachibura6040
    @brendachibura6040 Год назад +4

    Tuheshimu dini zetu kwasababu ndizo zinazotutengenezea Imani. Tujifunze kisikiliza kwa watu wengine sasa badala ya kubishana kuhusu dini embu tujifunze kupitia kwake huyu dada jmn

  • @julianamushi3392
    @julianamushi3392 Год назад +1

    🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️ngoja nije nikikimbia nikae kabisa nisikilize kwa utulivu

  • @dinapascal
    @dinapascal Год назад

    haleluya

  • @ilovejesus9303
    @ilovejesus9303 Год назад +2

    I love today's interview. Hongera sana dada Rose, endelea kumtumikia Mungu wako na kumuimbia.

  • @doricecyprian7246
    @doricecyprian7246 Год назад +1

    Amen

  • @rasmatty2000
    @rasmatty2000 Год назад

    Duh!!!

  • @jamesmaximillian7199
    @jamesmaximillian7199 Год назад

    🔥🔥🔥🔥🔥

  • @tithoobadia8361
    @tithoobadia8361 Год назад +1

    Mmh leo kazi ipoo😂

  • @dannylinguist15
    @dannylinguist15 Год назад +1

    GOD IS MIRACULOUS ❤️🙏

  • @victormwakipesile6990
    @victormwakipesile6990 Год назад +1

    Wakwanza

  • @reginakivinda8398
    @reginakivinda8398 Год назад

    besti naso

  • @mbwanamtessa8607
    @mbwanamtessa8607 11 месяцев назад

    We acha usanii rose, muongo kweli yesu kakutokea wapi!

  • @rehemangonji573
    @rehemangonji573 Год назад +1

    😂🤣🤣eeeh Leo hatar

  • @elingimiemakundi1229
    @elingimiemakundi1229 Год назад

    Mlete madam rita ,hamisa mobetto, mama dangote

  • @kennyndessa2039
    @kennyndessa2039 Год назад +5

    😂😂😂😂😂😂ata cjui nacheka nini😂😂😂

  • @alicenice1711
    @alicenice1711 Год назад +1

    Nataka kujuwa jina la Kislam la dada Rose

  • @poucostantin4403
    @poucostantin4403 Год назад

    Salama leo umeyakanyaga

  • @FreeGod368
    @FreeGod368 Год назад +4

    Hi ilileta utata ad Salama alichelewa kuipost

  • @ricky4843
    @ricky4843 Год назад

    Hii kamba

  • @HusseinMustafaParmar
    @HusseinMustafaParmar Год назад

    We should respect all religions as a Christian Tanzanian just said in the comment and if anyone has different views or debates or says the wrong of other faiths or argues with proof how they are wrong, he or she should not be hit at or stabbed as criminals in South Africa and elsewhere they do as the world is witnessing as here are animals and they don't have religion and others brought them terrorism too, but we should argue back or debate or leave him on his own if he won't come to truth or if his views are not right. The Tanzanian tolerance is because of its people and the Arabs who colonized it and lived there

  • @amanimanase8798
    @amanimanase8798 Год назад +2

    Na ndomaana nilikuwa najiulizaga kuhusu jina la MUHANDO mbona asili yake ni tanga lkn watu walinibishia sasa jibu wamelipata

  • @reetymutinda
    @reetymutinda Год назад

    The annointed one of God live long mom and may God bless you

  • @user-xf9or5cv1d
    @user-xf9or5cv1d Год назад

    Salma ushakua mzee una badilika kidogo kidogo tubia

  • @simas.a1003
    @simas.a1003 Год назад

    Aisee jaman, hadi nataka kulia

  • @eliassoingei2046
    @eliassoingei2046 Год назад +1

    Rose anajua mitaa ya Arusha balaa

  • @shilagijisandu3101
    @shilagijisandu3101 Год назад +3

    Leo kwa rose umeyakanyaga😂😂😂😂

  • @malapakipochi3317
    @malapakipochi3317 Год назад +5

    Waislamu hili linawauma kwelii kweli.....ni kama dini itawapeleka binguni.... lakini poleni waislamu na dini lenu la MAJINI..

  • @bedabenson6576
    @bedabenson6576 Год назад

    Lete Mgunda

  • @tantinebettynduwimana380
    @tantinebettynduwimana380 Год назад

    Kama huu angebaki kua mu Islam kama anavaa vizuri anajistiri😂😂😂😂

  • @charliestyles5535
    @charliestyles5535 Год назад +2

    Mkono mweusi 🤯

    • @gosbertgideon6843
      @gosbertgideon6843 Год назад +1

      Anazo alama za kumuonesha YESUKRISTO skuhyo kwaajili yake
      Je ww unazo alama

  • @sadikijani4307
    @sadikijani4307 Год назад

    Sio stori nzuri!! Nafikiri Salama usingeirusha hii!!!

    • @gosbertgideon6843
      @gosbertgideon6843 Год назад +2

      Imewakatakata maini wapngakristo

    • @nellymatalanga5033
      @nellymatalanga5033 Год назад +1

      Sasa utapangia salama maisha yake tengeza kipindi chako basi Salama hana roho mbaya kama nyinyi

    • @gosbertgideon6843
      @gosbertgideon6843 Год назад

      @@nellymatalanga5033 nashanga

    • @saxannjo6173
      @saxannjo6173 Год назад

      Ndio nyinyi wana wa IBILISI... Mnaumbuka sasa

    • @veeJesus
      @veeJesus Год назад +2

      Jamani waislamu mnaogopa hili JINA la YESU 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 hii itoshe kuwadhibitishia YESU sio nabii mtume wala apostle JESUS CHRIST is LORD ... YESU ni MUNGU

  • @javanwatson6675
    @javanwatson6675 Год назад +1

    mmh 10:15 - 10:20 hapo Rose alitaka atupige.. 🤠anyways I like her

    • @andrewdukho8795
      @andrewdukho8795 Год назад

      Hahaha

    • @andrewdukho8795
      @andrewdukho8795 Год назад

      Ijumaa ya majilio

    • @rozapetro1647
      @rozapetro1647 Год назад +1

      Hello get serious hayajakukuta cku hiyo ikitokea utaamn ya Rose
      Hii stor huwa anaisimulia sana..so co uongo

    • @javanwatson6675
      @javanwatson6675 Год назад

      @@rozapetro1647sijasema kua story yake ni ya uongo ila kweli mkristo hajui hata IJUMAA KUU, mimi ni shabiki wa Rose ila hapo amenipiga na kitu kizito

    • @ichicarodan6931
      @ichicarodan6931 Год назад

      Kwan Ijumaa kuu ipo kwny biblia, mbona wasabato hawajui coz hawasherekei

  • @familylove5417
    @familylove5417 Год назад +3

    Salama hoiiiii Leo🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 sura yake tu inaongea hiki kibibi kiongo sna 🤣🤣🤣

    • @tumlakimwaitumule
      @tumlakimwaitumule Год назад +1

      Shame on you,we utakua kijana forever sio? 🚮🚮

    • @ninjaisma7983
      @ninjaisma7983 Год назад

      Anatupanga anajifanya yeye nshapu kitengeza story za mungu.. ati mkaka mmoja katumwa na mungu daah Rose ww mshirikina mbayaa😅

    • @tantinebettynduwimana380
      @tantinebettynduwimana380 Год назад

      😂 😂 😂 😂 😂 😂

  • @maabadmmanga2896
    @maabadmmanga2896 Год назад +3

    Inalilah Waina Ilah Raghun Unatoka Ktk Dini Sahihi Dah Allah Akbarrrrrrr

    • @finiaskalist747
      @finiaskalist747 Год назад

      Mmwanza sasa😆😆😆

    • @FreeGod368
      @FreeGod368 Год назад +1

      Mwaka huu mtachonga viazii

    • @francesmpangwa8801
      @francesmpangwa8801 Год назад +1

      Ingekua dini yenu sahihi Mungu angemwambia aimbe Qaswida kwen mbwa wewe Yani mnapendaga kutuchokonoa sana wakristo

    • @gosbertgideon6843
      @gosbertgideon6843 Год назад

      Mtajua hamjui uislam ulikuja kumpnga kristo so kaeni kwakutulia chek nuru iliyoko kwake huwez kuipata

    • @gosbertgideon6843
      @gosbertgideon6843 Год назад

      @@francesmpangwa8801 mjinga huyu achana nae wana dini sahh lkn hata sku1 hajawahi kujidhihilissha kwao hata sku1 kujifunua imekua ngumu

  • @aminaomary5567
    @aminaomary5567 Год назад +3

    Dada ludi katika dini yako,madam umeshapona,mungu atakusaidia tu,pesa ulizozipata fanta biashara.

  • @makavelihassani9694
    @makavelihassani9694 Год назад +1

    Naheshimu tuu kipaji chako cha uimbaji dada rose!!!! Lkn si kwa upuuzi km huu ambao umeuzungumza.

  • @munirsalman5910
    @munirsalman5910 Год назад +7

    Series zaidi ya prison break🤣🤣🤣

    • @FreeGod368
      @FreeGod368 Год назад +3

      Mwaka huu mtachonga viazii waislamu chuki kibaao baki Dini yako

    • @abdulraufmohammedsalum6806
      @abdulraufmohammedsalum6806 Год назад

      @@FreeGod368 Dini yenu ya mchongo

    • @FreeGod368
      @FreeGod368 Год назад +1

      @@abdulraufmohammedsalum6806 We mwehu mi sina TIME naww kafie mbere 😂sijib watu walochanganyikiwa mimi

    • @abdulraufmohammedsalum6806
      @abdulraufmohammedsalum6806 Год назад +1

      @@FreeGod368 Tulia ww 😂😂

  • @josephngowoambroce418
    @josephngowoambroce418 Год назад +4

    hahahaha...MUONGO saaana Rose... ila unajua kuimba

    • @gracewairimu800
      @gracewairimu800 Год назад

      Mbona unasema nimuongo jaman

    • @annajustin1945
      @annajustin1945 Год назад +4

      Uongo wake nn kusema ushuhuda wa kweli?

    • @petermarash3705
      @petermarash3705 Год назад +1

      Mungu akusamehe

    • @christinewomanoffaith5479
      @christinewomanoffaith5479 Год назад +1

      We ndo unajua maisha yake?
      Ila watu bwana!

    • @HusseinMustafaParmar
      @HusseinMustafaParmar Год назад

      Tanzanian spirit if someone did wrong they say: May God forgive you. And encourage repentance and love and helping sinners leave sin as all are same in sin. The Prophet Muhammad is saying : All Humans Are Sinners But The Best Of Those Sinners Are Those Who Repent. I learned this Hadith from Sheikh Khalfan, Sheikh Saleh and Sheikh Kibriti when I was sleeping at manyema mosque when he knew me there and was good to me when he helped me some little change and these days when I said I am with Christian in 2017 he helped me some little change even taking me as a Preacher like himself but knows me since small as an orphan childn

  • @mrfashion1687
    @mrfashion1687 Год назад +7

    🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Rose katupiga na kitu kizito kichwani

    • @FreeGod368
      @FreeGod368 Год назад +2

      Mwaka huu mtachonga viazii

    • @gosbertgideon6843
      @gosbertgideon6843 Год назад +2

      Kivp
      Haya maono yapo nayy sio wakwanza uamn usiamn hyo ndio YESUKRISTO mwana wa Mungu aliyehai ambaye alikufa na kufufukq

    • @wisemelodytz589
      @wisemelodytz589 Год назад +1

      Umepigwa peke ako bro

    • @albogastmselejr4583
      @albogastmselejr4583 Год назад

      Wee Nae Ngoja Siku Yakukute Ndo Utakuja Kuona Kwamba Rose Muhando Anaongea Kweli Bado Hujaanza Kuishi Wewe

    • @magdalenajoel4409
      @magdalenajoel4409 Год назад

      Jisemee ww usitujumlishe sisi

  • @ommylamsa1236
    @ommylamsa1236 Год назад

    una miaka 12 na dini ya kiislamu unaijua vizuri alafu ujui yesu ni nani....unataka uende kwake ukamuone😶

  • @tantinebettynduwimana380
    @tantinebettynduwimana380 Год назад

    Mtu akitaka kutoka kwenye uislam mpaka aseme Yesu alimtokea dah waislam tuna shida sisi tunamkubali Yesu sababu na yeye anamuabudu Mwenyezi Mungu wa pekee

  • @robartifabiani
    @robartifabiani Год назад +2

    Kumbe yesu ni mzungu🤔

  • @stevewanga957
    @stevewanga957 Год назад +7

    Uislamu ndio njia ya haki mbele ya Mwenyezi Mungu..

    • @FreeGod368
      @FreeGod368 Год назад +8

      Hatuna cha kukusaidia hatuko kwenye kampen ya DiNI

    • @stevewanga957
      @stevewanga957 Год назад +1

      @@FreeGod368 uzury ni maoni yangu binafsi

    • @FreeGod368
      @FreeGod368 Год назад

      @@stevewanga957 Ni swala muda tu kuelewa Yesu ni nan? Mi najiulizaga iv nisingezaliwa mkristo iv ningekuwa muislamu kabisaaa? 🥹😓Yaam stakag kuamin nampenda Yesu yy ni halisi so wakuhis his tu kama hewa ukiMuomba unashuhudia mafunuo ndotoni , au ya waziwazi ndio apooo tu napopenda Dini yangu, mim nmewai amka nkaomba dakika 5 Mungu akaniambia hi sim itaibwa Leo nkastuka nkaombea dakika 1 na io sku sim yangu kidooogo iende nkakumbuka Mungu aliniambia nisingeomba ingeenda huyo ndie Mungu naemjua mimi asiebubu na mengine meengi leo hi nabadil vipDini mimi nakichaa, Magufuli kafa tarehe 17/3 mimi tarehe 2/2 nkua shaona kifo cha magu na sababu vile vilee leo hi vip nache kuamini Dini yangu Ambae Mungu hunifunulia ya sirini

    • @stevewanga957
      @stevewanga957 Год назад

      @@FreeGod368 ww wamtambua Yesu kama nani?

    • @FreeGod368
      @FreeGod368 Год назад

      @@stevewanga957 Mwana wa Mungu so kama nabii wala mtume Yesu ni zaid ya mjumbe wa Mungu na pia Yesu kama mwana wa Mungu biblia ni Mungu pia mfano uez sema ndama so ng'ombe namimi naamini sabab ya maandiko tofaut tofaut na zaid ya hapo pale Yesu anaelezea jinsi yeye na baba walikuepo kabla ya kuumbwa ulimwengu akiwa anamsaidia kazi ya uumbaji

  • @ninjaisma7983
    @ninjaisma7983 Год назад

    Uyu dada muongo sanaa afu mshirikina sana..ati mungu anakujibu baada ya miaka kadhaa😅😅😅 story yako haimake sense

    • @magdalenajoel4409
      @magdalenajoel4409 Год назад

      Kaa Kwa kutulia ww acha mungu afanye kazi yake

    • @sarahgaula2220
      @sarahgaula2220 Год назад +1

      Kwani Mungu anajibu baada ya miaka mingapi? Mana mi nimekaa miaka 15 ya ndoa na mume wangu akaota Nina ujauzito na wiki lililofuata nikaingia siku za hatari nikapata ujauzito na nimejifungua Nov 15, 2022

  • @seinabelimi2296
    @seinabelimi2296 Год назад +4

    yani wewe km yesu alikupenda ungezini nje na kuzaa watoto haramu hv kweli inaingia akilin hebu rudi ktk dini yko tubia madhambi yko wacha kutupiga na vitu vizito 😅😅😅🤣🤣

    • @gosbertgideon6843
      @gosbertgideon6843 Год назад +1

      Mtapata tabusana

    • @tuliadamson3422
      @tuliadamson3422 Год назад +7

      @@gosbertgideon6843 kunamdada alikua mzinzi kwenye biblia alipaka machozi yake kwenye miguu ya yesu uku akiomboleza yesu akasema nawataka watu kama hawa kulikowale wanaojifanyaa sio watenda dhambi. Tunapojielekeza kwa yesu sio kwamba ni wasafi na hatuna dhambi bali ni kwa sababu tunadhambi nyingi hatujui n jinsi gani tutatoka hivo tunamfata yeye tupate msaada kwake.

    • @gosbertgideon6843
      @gosbertgideon6843 Год назад

      @@tuliadamson3422 amen

    • @neemakikoti5091
      @neemakikoti5091 Год назад +3

      Usihukumu usije ukahukumiwa

    • @ndojes711
      @ndojes711 Год назад +1

      We unajiona UMEKAMILIKA......! Hakuna mkamilifuuuuuu,. Hata ufanye DHAMBI maelfu MWENYEZI MUNGU NI MWINGI WA REHEMA,. Kwanza kakojoe ULALE hukoooo HUNA MBINGU YA KUMPELEKA

  • @aishaomarry6996
    @aishaomarry6996 Год назад +2

    Yesu ni mwana wa Mungu? ???? Mungu anazaa?????

    • @apolinarytheking
      @apolinarytheking Год назад

      Hata wew

    • @apolinarytheking
      @apolinarytheking Год назад

      Hata wew

    • @neemakikoti5091
      @neemakikoti5091 Год назад

      Kwani wewe unanafsi ngapi?

    • @neemakikoti5091
      @neemakikoti5091 Год назад

      Mungu Ni mmoja Ila ananfsi tatu Mungu Baba Mungu mwana Yesu na Mungu Roho mtakatifu kwa hivyo Yesu Ni Mungu maana yupo katika ndani ya uungu

    • @sylvesterhezron8062
      @sylvesterhezron8062 Год назад +1

      Ndiyo Aisha Mungu anazaa ila siyo kwa njia ya kibaiolojia ni kwa njia ya imani anatuzaa

  • @amirymdee4259
    @amirymdee4259 Год назад

    ***Kumbe Yesu ni mzungu ndo nimejua Leo***

    • @FreeGod368
      @FreeGod368 Год назад +2

      Mamako kumbe ni Mngoni nimejua Leo

    • @FreeGod368
      @FreeGod368 Год назад +1

      Muhammad kumbe ni mzaramo nimejua leo , make wazaramo wengi waislamu

    • @rozapetro1647
      @rozapetro1647 Год назад

      Hey ppo, if you're not sure of what to type you better don't

    • @sarahgaula2220
      @sarahgaula2220 Год назад

      @@FreeGod368 😳 He!

  • @G.r.e.a.t.I.Q
    @G.r.e.a.t.I.Q Год назад +3

    Kumbe, ndo maana... Walikupatia ukiwa akili bado haija unga. Hukuwa unajua lolote juu ya ulicho kifanya...juu ya kutoka ndani ya UISLAM!
    Ibilisi alikujia mzima mzima. Hukujua, vile ulikuwa mtoto. Hukua na elimu juu ya njama zake za kuwarubuni watu kuwa upande wake!

    • @bernadetamodest6170
      @bernadetamodest6170 Год назад

      Acha usenge kwan kuwa mkristo ni uibilis,wewe ambaye huingiliw na ibilis unapaaa au vp,yawezekan wewe mashetan ya kufuga ni wewe,kwa waganga ni wewe,mchaw ni wewe lakin unahukumu wenzako kwenye uhuru wao wa kusalu na kuabudu.Shindwaaaaaaaaaaaaaaaaa

    • @G.r.e.a.t.I.Q
      @G.r.e.a.t.I.Q Год назад

      @@bernadetamodest6170 hebu kwanza meza dozi yako ya kule MIREMBE kabla hujaanza kufanya kazi ya kusafisha majalala bila malipo.

    • @bernadetamodest6170
      @bernadetamodest6170 Год назад

      @@G.r.e.a.t.I.Q Ameze nan sasa mimi au wewe hapo mjinga mmoja usiyejielewa,?shetan na robo! pumbavu kabisa,unaongea tu kama unaharisha,fukara wa fikra. Mixuuuuuuuuuuuuu

    • @G.r.e.a.t.I.Q
      @G.r.e.a.t.I.Q Год назад

      @@bernadetamodest6170 na wewe unaye tukana ni nani? Mpumbavu, siyo? Au umekosa Macintosh kwenu? Kama huwezi mijadala mitandaoni basi ntamaza tu. Usitukanishe waxes wako wakaonekana hawakukulea vyema. Ilhali wewe ndo umekacha madunzo yao mema. Wacha ukosefu wa adabu!
      Ukiona haiku changiwa vile ungependa basi Changia vile ambavyo yule aliye kuvunja moyo aelewe. Tu kama ulipata malezi na maadili mema kwa wazazi wako.

    • @bernadetamodest6170
      @bernadetamodest6170 Год назад

      @@G.r.e.a.t.I.Q Ni kweli kabisa wewe uliyesema kichaa sijui mirembe hukutukana ,you was very perfect.Mijadala ndiyo kama hiyo ukimtukana mtu maharage yeye atakuita mchicha au chainiz so usifikir utakuwa salama kwa kutukana wenzako nao wakuache,sahau hiyo kitu.