MITUNGI YA GESI KUUZWA KWA BEI YA RUZUKU,WANASINGIDA KUNUFAIKA
HTML-код
- Опубликовано: 6 фев 2025
- Katika kuziwezesha kaya za vijijini na mijini kuhakikisha zinatumia nishati safi ya kupikia,Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), itatoa mitungi ya gesi 19,530 yenye ruzuku kwa Mkoa wa Singida ambayo itauzwa kwa bei ya chini ya Sh.20,000 kwa mtungi mmoja.
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Halima Dendego, akizungumza leo (Disemba 4,2024) baada kupokea maafisa kutoka REA ambao wameleta mradi wa usambazaji wa mitungi ya gesi yenye ruzuku, alisema mitungi hiyo itagawiwa kwa uwiano sawa katika wilaya zote tano za Mkoa wa Singida.