HUYU NDIYE MGONJWA AMELAZWA KCMC KWA MIAKA 8, MFULULIZO /ANATUMIA OKSIJENI MAISHA YAKE YOTE

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 14 окт 2024
  • Tumaini Minde (21) anaweza kuwa mmoja wa wagonjwa aliyelazwa kwa muda mrefu zaidi katika hospitali ya Rufaa ya KCMC baada ya kulazwa katika hospitali hiyo kwa miaka 8 sasa mfululizo tangu mwaka 2013.
    Kwa sasa Tumaini ambaye alilazwa KCMC akiwa na umri wa miaka 14, anatumia mitungi miwili ya hewa ya Oksijeni kwa kila saa 24, na mtungi mmoja hujazwa hewa hiyo kwa Sh45,000 sawa na Sh90,000 kwa siku.
    Mama yake mzazi, Florah Minde, amelazimika kuhamishia makazi yake katika hospitali hiyo kwa miaka 8 akimuuguza mwanae na akisha mhudumia ,hutoka wodini na kwenda kutafuta vibarua ili apate fedha ya kujikimu.
    Mwananchi Digital limefanya mahojiano na Bibi Florah na hapa anaeleza mwanzo mwisho namna mwanae alivyoanza kuugua hadi sasa ambapo kitanda cha hospitali KCMC kimeguka kuwa makazi yao.
    Baadae Florah akaeleza namna mwanae anavyopenda kutazama movie kupitia simu yake ya kiganjani na asipompakulia movie mpya, siku hiyo hapatatosha kwani atalia usiku mzima.
    Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Gabriel Chisseo naye akazungumzia mgonjwa wao huyo kama anavyoeleza
    Mpenzi mtazamani wa Mwananchi Digital, kama umeguswa na madhila anayopitia kijana Tumaini pamoja na mama yake, basi unaweza kutuma msaada wako kwa Florah kupitia nambari ya Mpesa 0769152848

Комментарии • 8

  • @ramadhanimbulu6716
    @ramadhanimbulu6716 4 года назад +2

    Pole mama! Radhi za mungu na pepo ya Mungu IPO chini ya nyayo za mama zetu. Tuwapende mama zetu na kuwaheshimu..!!

  • @fekechezidg2036
    @fekechezidg2036 4 года назад +2

    Pole jamani mungu atakujalia

  • @fallymetoo191
    @fallymetoo191 4 года назад

    Lahaula walakuwata illah billah. M.mungu ni muweza wa kila jambo.
    Pole sana mama kwa unayoyapitia. Ila tunamuomba M.mungu amfanyie wepesi MJA wake huyo. INSHALLAH 🤲

  • @alicempuya5238
    @alicempuya5238 4 года назад

    Mungu mponye kwa mkono wake wa pekee

  • @happinessmosala2217
    @happinessmosala2217 3 года назад

    Mungu akamfanyie wepesi apone 👃👃👃

  • @rajabumlaluko2897
    @rajabumlaluko2897 3 года назад

    Sad moment

  • @emanuelmwanga4
    @emanuelmwanga4 4 года назад

    Jamani watu wanateseka ee mungu amponye tu dahh