HABARI WANYAKYUSA NA WADAU WA WANYAKYUSA*( MUGONILE MWESA)!

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 17 ноя 2024
  • UONGOZI WA #MAKUMBUSHO YA TAIFA UMETOA NAFASI KWA JAMII YA #WANYAKYUSA KUANDAA #TAMASHA LA KITAIFA LA UTAMADUNI JULAI, 2024.
    Kundi hili ni maalumu Kwa ajili ya Kuandaa na kuratibu shughuli za Tamasha la Wanyakyusa litakalo fanyika tarehe 26, 27, na 28 Julai, 2024 ktk Kijiji Cha Makumbusho DSM.
    #Mkutano wa Kwanza wa Wanyakyusa Wote Kwa ajili ya kuratibu Tamasha utafanyika tarehe 23, March, 2024, saa 9 Alasiri eneo la Kijiji Cha Makumbusho DSM, ukiongozwa na Mgeni Rasmi wa Mkutano Architect: Elius Mwakalinga* ambapo Mkutano huo utakamilisha kuunda Kamati zote za Tamasha na kuandaa Mkutano wa kufanyika Mkoani Mbeya utakao oongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
    Kundi hili linabeba Mnyakyusa yeyote Toka mahali popote Duniani. Lengo ni kuonesha Mila na Utamaduni wa Wanyakyusa Ili kuuendeleza na kuacha Alama za Urithi Kwa Kizazi kingine (Makumbusho ya Taifa wanajukumu la kuhifadhi haya). Lakini pia Tamasha hili *litazindua Nyumba za Asili za Wanyakyusa zilizojengwa Kijiji Cha Makumbusho DSM*.
    Mara ya Mwisho Tamasha kama hili la Wanyakyusa lilifanyika miaka ya 1990s. Hivyo tunategemea UMOJA wetu wa Kizazi hiki utakusanya taarifa zote za Mila, desturi, Tamaduni, vyakula na Vinywaji Ili viingie kwenye Uhifadhi Rasmi Makumbusho ya Taifa.
    Tukio hili ni kubwa na muhimu sana hivyo bajeti yake inategemea kufikia Tsh. million 350 ambazo zitakusanywa kupitia Akaunti ya serikali ya Makumbusho na zitatolewa Kwa idhini ya Vikao vya Kamati.
    Ni tarajio la maandalizi haya kuwasafirisha wageni 400 Toka #Kyela, #Rungwe na #Mbeya mjini* ambao ni Vikundi vya #Ngoma ( Mang'oma, Samba, Kitombwike, Magosi, Kapote, Mababatoni, Mang'olong'ondo, Kibwenga, Ndingala) wakiambatana na viongozi wetu wa Jamii zetu yaani Machifu na wazee wa Mila nk.
    #Karibuni nyote kufanikisha jambo hili muhimu Kwa Jamii ya #Wanyakyusa
    chat.whatsapp....

Комментарии •