Putin ataka Kamala Harris kumshinda Trump, Vifo vikizidi kuongezeka Ukraine

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 15 сен 2024
  • Rais wa Russia, Vladimir Putin, amedai kuwa anamtaka mgombea maalum, Kamala Harris, kushinda uchaguzi wa urais wa Marekani unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba 2024.
    Akizungumza katika Jukwaa la Uchumi wa Mashariki, alieleza kuwa Kamala Harris, ambaye ni mwanademokrasia, ndiye chaguo lililopendelewa na Russia, akisisitiza kuwa kicheko chake 'kinachoambukiza' ndicho sababu ya kumchagua badala ya Donald Trump.
    Hata hivyo, kauli hizo zilionekana kama dhihaka, kwani Putin na Trump wamekuwa wakipongezana kwa muda mrefu. Ushindi wa Trump, mgombea wa chama cha Republican na Rais wa zamani wa Marekani, huenda ukasababisha kupungua kwa misaada kwa Ukraine, ambayo imekuwa ikisaidia nchi hiyo kupambana na Russia tangu mwaka 2022.

Комментарии •