Mikopo umiza ni kikwazo / Wananchi wahimizwa kujiandikisha kupiga kura. "Elimu jamii"

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 6 сен 2024
  • Wito umetolewa kwa wananchi wa Tanzania kuwa na hofu ya Mungu pamoja na kujitokeza kuboresha na kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
    Wito huo umetolewa na Padre Frolence Rutaihwa, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Kiuchungaji Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC, katika Semina elekezi juu ya elimu ya masuala ya uraia, wajibu na haki katika maisha ya mwanandamu mkutano uliofanyika katika ukumbi wa BCD STELLA Hotel Jimbo Katoliki la Bukoba.
    Padre Rutaihwa amesema kuwa mambo mengi yanaharibika kwenye jamii ya sasa, sababu ya baadhi ya wananchi kukosa hofu ya Mungu jambo linalopeekea kuwe na matukio ya ajabu na kuwataka wazazi kuwa na malezi bora kwa watoto na kuwafundisha sala ili kujenga dhamiri inayofaa kwa watoto wao inayoweza kuepuka mauaji, ugomvi na chuki katika jamii.
    Aidha Padre Rutaihwa amesema kuwa Tanzania inapoelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni haki ya msingi kwa kila mtanzania kujiandikisha na kupiga kura kikamilifu na kuwataka viongozi kutanguliza maslahi ya taifa na sio maslahi binafsi ili kuleta maendeleo katika taifa na kuwasisitiza wananchi kuwaibika ipasavyo katika katika jamii yake.
    Badhi ya washiriki waliohudhuria mafunzo hayo akiwemo mtaalamu wa lishe Dkt Magdalena William amesema kuwa ili kuwa na uchumi bora na imara wananchi wantakiwa kupata lishe bora na ulaji unaofaa ili kupata mlo kamili na kubainisha kuwa mama wajawazito wanashauriwa kula vyakula yenye madini ya zink ili kumpa lishe bora mtoto aliyetumboni kabla ya kuzaliwa.
    Naye Katekista Joseph Rweyendera wa Parokia ya Kagondo ameishauri jamii kujiunga na vikundi vya mikopo nafuu kupitia taasisi za benki ili kuepuka mikopo umiza maarufu Kausha damau ambayo imekua ikisababisha ndoa nyingi kuvunjika sababu ya riba ambayo sio rafiki kwa wafanyabiashara wadogo.
    www.radiombiu.co.tz
    #RmSautiYaFaraja

Комментарии •