KIPENZI Zama na si zama sana, alipapatika, Kimwana wapi ‘tamwona, akahuzunika, Mawazo yalikinzana, akahangaika, Na wengi aliwaona, waliosifika, Kama bara kuna barafu, joto pwani sihimili. Alisaka kinyemela, hakumpata, Mwenye jina Cinderela, akamf’ata, Kumbe alipenda hela, hayo matata, Tungule hawezi kula, huyo ‘kapita, Kama bara kuna barafu, joto pwani sihimili. Kinyerenyere ‘kasaka, Unguja hadi Pemba, Wal’oumbwa ‘kaumbika, tena was’o washamba, Wahindi na Wamerika, wa kiuno chembamba, Mombasani ‘mefurika, wa mapozi na pamba, Kama bara kuna barafu, joto pwani sihimili. Toka Pemba k’enda Kenya, nchi ya jadi, Pwani kote akapenya, kuf’ata sudi, Wengi wakamsengenya, hao hasidi, Ijapo walimsinya, alikaidi, Kama bara kuna barafu, joto pwani sihimili. Kusini mbali kaenda, nchi in’osifika, Akidhani kuna tunda, tamu lenye kulika, Wazulu akawapenda, hasa wal’oumbika, Un’otaka watatenda, ila yapo mashaka, Kama bara kuna barafu, joto pwani sihimili. Kitandani akiwaza, usingizi ‘kamsepa, ‘Kabaki kujiuliza, yuko wapi wa kujipa? Muda wote kapoteza, kwa mawazo yas’olipa, Kama bara kuna barafu, joto pwani sihimili. Hatimaye kaibuka, Malkia wa upendo, Moyoni alipofika, aka’nza legeza fundo, Suraye ya malaika, ‘tadhani mwana mitindo, Ama bara kuna barafu, joto pwani sihimili,
KIPENZI
Zama na si zama sana, alipapatika,
Kimwana wapi ‘tamwona, akahuzunika,
Mawazo yalikinzana, akahangaika,
Na wengi aliwaona, waliosifika,
Kama bara kuna barafu, joto pwani sihimili.
Alisaka kinyemela, hakumpata,
Mwenye jina Cinderela, akamf’ata,
Kumbe alipenda hela, hayo matata,
Tungule hawezi kula, huyo ‘kapita,
Kama bara kuna barafu, joto pwani sihimili.
Kinyerenyere ‘kasaka, Unguja hadi Pemba,
Wal’oumbwa ‘kaumbika, tena was’o washamba,
Wahindi na Wamerika, wa kiuno chembamba,
Mombasani ‘mefurika, wa mapozi na pamba,
Kama bara kuna barafu, joto pwani sihimili.
Toka Pemba k’enda Kenya, nchi ya jadi,
Pwani kote akapenya, kuf’ata sudi,
Wengi wakamsengenya, hao hasidi,
Ijapo walimsinya, alikaidi,
Kama bara kuna barafu, joto pwani sihimili.
Kusini mbali kaenda, nchi in’osifika,
Akidhani kuna tunda, tamu lenye kulika,
Wazulu akawapenda, hasa wal’oumbika,
Un’otaka watatenda, ila yapo mashaka,
Kama bara kuna barafu, joto pwani sihimili.
Kitandani akiwaza, usingizi ‘kamsepa,
‘Kabaki kujiuliza, yuko wapi wa kujipa?
Muda wote kapoteza, kwa mawazo yas’olipa,
Kama bara kuna barafu, joto pwani sihimili.
Hatimaye kaibuka, Malkia wa upendo,
Moyoni alipofika, aka’nza legeza fundo,
Suraye ya malaika, ‘tadhani mwana mitindo,
Ama bara kuna barafu, joto pwani sihimili,
🎉👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾🤝🤜🏻🤛🏼🙏thank you brother for the good poem
❤
Lit brother