JANGA LA MOTO LOS ANGELES NGOMA BADO MBICHI, VIFO VYAFIKIA 24

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 12 янв 2025
  • Hali mbaya ya hewa inayochangia upepo mkali inatajwa kuchangia moto huo kutodhibitiwa, huku vifo vilivyosababishwa na moto huo vikifikia 24.
    Los Angeles. Moto wa nyika umeendelea kuwa mwiba kwa wakazi ma maofisa wa Kikosi cha Zimamoto jijiji Los Angeles nchini Marekani baada ya vifo kuongezeka na kufikia watu 24.
    Zimamoto pia imetahadharisha kuwa huenda idadi ya waliofariki kutokana na moto huo ambao uliibuka Januari 9, 2025, ikaongezeka kwa kile kinachotajwa bado ufuatiliaji unaendelea kujua madhara katika maeneo ambayo bado unaendelea kuteketeza.
    Tovuti ya BBC imeripoti kuwa wakati huu ambao jitihada za kuudhibiti hazijazaa matunda, kunahofiwa kuibuka upepo mkali hususan eneo la Santa Ana kuanzia jana Jumapili hadi Jumatano wiki hii utakaokuwa ukivuma kwa wastani wa kasi ya Kilometa 96 kwa Saa.
    Pamoja na moto huo kuendelea kuteketeza maeneo ya vilima vya Hollywood, jitihada za Zimamoto zinaonekana kuzaa matunda baada ya kuupunguza nguvu hususan katika maeneo ya Palisades na Eaton.
    Tayari maofisa wa zimamoto kutoka nchini Marekani wameongezewa nguvu na mamia ya wataalam wa kuzima moto kutokea nchini Canada na Mexico, ambao wameendelea kuwasili nchini humo.
    Ofisi ya Usimamizi wa Afya jijini Los Angeles imetoa taarifa kuwa waliofariki hadi leo Jumatatu Januari 13, 2025, ni watu 24 huku 16 wakiwa hawafahamiki waliko.
    Kati ya waliofariki, watu 16 waliteketea katika moto uliounguza eneo la Eaton, huku nane wakifariki katika moto uliounguza eneo la Palisades jijini humo.
    Hadi sasa kuna moto katika maeneo matatu ya Jiji la Los Angeles ambao bado ni tishio kwa raia nchini humo.
    Moto mkubwa kati yake uko eneo la Palisades, ambao takwimu za zimamoto zinaonyesha hadi sasa umeteketeza ekari zaidi ya 23,000 huku asilimia 11 ya moto huo ikiwa imedhibitiwa.
    Moto uliozuka eneo la Eaton jijini humo unatajwa kuwa wa pili kwa ukubwa ba hatari ambapo hadi leo umeteketeza ekari 14,000 japo asilimia 27 imeshadhibitiwa.
    Takwimu zinaonyesha kuwa moto ulioibukia eneo la Hurst kwa takribani ekari 799 umekaribia kudhibitiwa na kuzimwa kabisa katika jitihada za vikosi vya Zimamoto kutoka mataifa hayo.
    Jana Jumapili, Taasisi Binafsi ya Utabiri ya Accuweather ilidai kuwa hasara iliyosababishwa na moto huo katika mali na makazi huenda ikawa imefikia kati ya Dola za Marekani 250 bilioni (Sh631.25 trilioni) Dola 275 (Sh694.37 trilioni).
    Mamlaka hiyo pia imeonya hatari ya moto huo kusambaa maeneo mengi ya Jimbo la Los Angeles endapo upepo unaotarajiwa utapuliza kwa kasi na usipodhibitiwa kwa wakati hivyo kuwataka wananchi kuongeza umakini wakati huu.
    "Kwa bahati mbaya tunalazimika kutoa taarifa mbaya kuwa huenda tukapitia wakati ambao kuna moto wenye madhara zaidi katika kipindi cha Jumapili hadi Jumatano kutokana na upepo unaotarajiwa kupuliza katika siku hizo," Mkuu wa Zimamoto eneo la Pasadena, Chad Augustin ameieleza BBC.
    "Pamoja na kuwa tunaendelea kuudhibiti ila hakuna dalili za kuushinda hadi sasa,” amesema.
    Kristin Crowley, ambaye ni Mkuu wa Zimamoto jijini Los Angeles, amewataka wananchi ambao wameondolewa katika makazi yao kutorejea katika eneo hilo wakati huu hadi pale itakapotangazwa vinginevyo.
    Mkazi wa Bonde la Topanga jijini humo, Alice Husum, (67) ameieleza BBC kuwa kuna moto ambao umeonekana kuibukia eneo hilo usiku wa kuamkia leo jambo ambalo limeibua taharuki kwake na majirani zake juu ya hatma ya makazi yao.
    Jana Zimamoto walifanikiwa kuudhibiti moto huo usifike ulipo msitu wa Taifa hilo uliopo Los Angeles, eneo ambalo ndiko kuna Kituo cha Taifa cha Usafirishaji wa Anga.
    Takwimu zinaonyesha watu 29 wanashikiliwa kwa madai ya kufanya uharibifu na udokozi wa mali za waathiriwa wa janga hilo hususan ni maeneo ambayo wakazi wametakiwa kuondoka.
    Mkuu wa Jeshi la nchi hiyo jijini Los Angeles, Robert Luna amesema ulinzi umeimarishwa kwenye eneo lenye makazi ya waathiriwa wa moto huo na tayari askari wa Jeshi la nchi hiyo zaidi ya 400 wamemwagwa eneo lote kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.
    Gavana wa California, Gavin Newsom ametangaza kuwa askari wa jeshi la nchi hiyo 1,000 wataongezwa ili kuimarisha usalama katika eneo hilo.
    Hadi sasa maofisa wa Zimamoto zaidi ya 14,000 wamefika eneo la Kusini mwa California, wakisaidiwa na ndege 84 na mashine za kuzima moto 1,354.
    Idadi ya waliomriwa kuyaacha makazi yao inakadiriwa kuwa ni watu 105,000 huku zaidi ya 87,000 wakiwa hatarini kutakuwa kupisha makazi yao kutokana na tishio la moto huo.
    Msimamizi wa Ofisi ya Wakala wa Uratibu wa Majanga (Fema) nchini humo, Deanne Criswell, amesema bado kuna tishio la moto huo katika usalama wa binadamu.
    Imeandikwa na Mgongo Kaitira kwa msaada wa Mashirika.

Комментарии • 22

  • @HanifaOman-oo4pl
    @HanifaOman-oo4pl 9 часов назад +2

    Mmevuna mlichokipanda. Kwaraha zenu. 😂😂

  • @JoshuaJoshua-t7r
    @JoshuaJoshua-t7r Минуту назад

    Poleni wamarekani kwa janga kubwa kikubwa pamoja na jitiada za kuzima tumwombee mungu msamaha kwani hatujui tunakosea wapi

  • @selemankishema5780
    @selemankishema5780 8 часов назад +1

    Dunia nzima haina amani kwa ajili ya hawa viumbe wache Allah awastue kwa yupo labda watastuka

  • @AliNassor-qt6fm
    @AliNassor-qt6fm 9 часов назад +1

    😂😂😂😂😂😂😂acha waipate

  • @samratsultan9055
    @samratsultan9055 8 часов назад +1

    Mung atuepushie na sisi amin

  • @HabibuUrasa
    @HabibuUrasa 7 часов назад

    Mpaka waseme kwanini wamebomoa gaza Mungu yupo pamoja na wenye kudhulumiwa

  • @Fatma-h7t9g
    @Fatma-h7t9g 43 минуты назад

    Tenda wema atalipwa wema na tenda uovu atalipwa uovu. Mkome kuisaidia Israel. Bado kabisa balaaa linakujieni

  • @selvestarjoseph2649
    @selvestarjoseph2649 59 минут назад

    Kwan uwo moto umetokana nanini et mbona mashindwa elewa😢

  • @UstadhiAdnani-q8u
    @UstadhiAdnani-q8u 5 часов назад

    Mmemwaga sana damu za wasio na hatia zinawatafuna

  • @mozamoza3960
    @mozamoza3960 10 часов назад +1

    Huja Waka bado una kongwa

  • @rikekikonyo2265
    @rikekikonyo2265 9 часов назад

    Kufeni tu mahayawani nyie😊

  • @hassaniabdi3991
    @hassaniabdi3991 9 часов назад

    Wacha walipe na waoo wajiu majanga ya kushambukia mataifa yasio kua na nguvu

  • @UstadhiAdnani-q8u
    @UstadhiAdnani-q8u 5 часов назад

    damu za vichanga vya Gaza zinawatafuna ila nauliza mfumo wav THAAD uko wapi

  • @FatmaSalum-i1i
    @FatmaSalum-i1i 10 часов назад +2

    Mpaka wamjue alowaumba

  • @Drsilo-v5k
    @Drsilo-v5k 9 часов назад

    Ata badoo makufari hawa

  • @maryammaryamm9548
    @maryammaryamm9548 10 часов назад

    Mnaonjeshwa machungu n nyinyi kudogo tu mmeonyeshwa tu hivyo endeleeni kuonja radha hiyo bado haitoshi

  • @winifridabyesigwoa741
    @winifridabyesigwoa741 10 часов назад

    😊

  • @LupakisyoKandonga
    @LupakisyoKandonga 9 часов назад

    Ombeni musada musaidiwe

  • @JumaKumchalangwe
    @JumaKumchalangwe 9 часов назад

    Hii yenyewe ni muvitu sio jambo lakweli wanamzuga mrusi

  • @FatumaJuma-b2g
    @FatumaJuma-b2g 10 часов назад

    🙆🙆🙆🙆jmn mh