Sallam Afichua Walichokifanya WCB Baada Kufungiwa Na Media Zote Kubwa | SALAMA NA SALLAM SK PT 2
HTML-код
- Опубликовано: 18 янв 2025
- #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Sallam Sharaff ni lejendari, na hilo liko wazi kwa anayetaka na asiyetaka, kwa umuhimu wake kwenye maisha ya msanii nambari moja kwa sasa ni kama nywele, usipomkuta kichwani basi hata kwapani hatokosekana. Na kwa utashi wangu nadhani kama wana Bongo Flava au wasanii ambao ‘wako tayari kuwekeza’ basi wangemkimbilia kwa kasi ya 4G ilimradi wapate mawazo tu ya jinsi gani wanaweza kufanya ‘meli’ yao ifike na pale panapotokea mrama wajue wimbi gani la kuliepuka na wimbi gani ndo walipandie kwa juu.
Sallam si muongo na hili ninalijua kwasababu ni rafiki yangu, atakavyokuambia ndivyo lilivyo, Sallam anapenda pesa na hilo liko wazi na wala hajifichi nalo ila kubwa zaidi Sallam anapenda MAENDELEO. Ukitaka msielewane naye milele na milele basi onyesha nia au muonyeshe moja kwa moja kama unataka ’kumharibia’ mkate wake. Hakika hatokuacha salama. Atahakikisha unaenda na maji kwasababu mkate wake ndo maisha yake. Tofauti yake na wengi wetu ni kwamba wengi wetu tukijua mtu anataka kukuharibia basi na wewe utajificha au utamuepuka au utamchukia tu, Sallam yeye atakuonyesha waziwazi kama HAKUPENDI.
Muziki anaufahamu vizuri tu na mengine anayang’amua as we go kama binadamu wa kawaida, mapenzi yake kwa mziki huu na kwa kupenda anachokifanya ndo kunamfanya awe THE BEST MANAGER. Maisha na mipango na maendeleo ya msanii nambari moja kwa sasa yalianza kubadilika sana mara baada ya Sallam kuingia kazini, na ilibidi aanze kama International Manager maana kwa upande wa ndani tayari Babu Tale na Said Fella walikua washapatawala. Haikua kesi kwake, ambacho alikifanya ni kuhakikisha Diamond anapata collabo na show nyingi za nje ambazo yeye alikua anaenda naye. Wakati akiwa wanapokua alitumia nafasi hiyo kutengeneza network nyengine. Mipango yake na uwajibikaji na jinsi vitu vilivyokua vinasogea vilimfanya Platnumz ampende zaidi, amshirikishe kwenye mambo mengi zaidi ambayo matunda na malipo yake ndo haya ambayo wanakula leo na kesho na keshokutwa ilhali mimi na wewe tunashuhudia historia inavyozidi kuandikwa.
Kwa Said Fella kupata udiwani nako pia kulimfanya Sallam apate majukumu zaidi ya hata ya ndani sasa maana kipindi kile cha Hayati JPM kazi ilikua inabidi ifanyike na Sheikh Said alipigiwa kura na watu, so mara nyingi ilikua inabidi afanye kazi za kutumikia wananchi wake, na huku nyuma Sallam akawa anaezeka banda lake la kuishi kwenye ufalme wa Diamond Platnumz.
Nakumbuka mwaka 2018, London Town, Diamond alimaliza show zake na Sallam akabaki nyuma, kilichowapeleka kule ilikua ni show ambayo yeye Sallam, my cousin Dulla Meru na moja ya mapromota hodari kutoka Nigeria ambaye anaishi London Ndugu Smed waliiandaa, ilienda poa na naamini ile ilifungua milango mingi sana. Alibaki nyuma kuhakikisha mambi yote yanakwisha freshi na pia kutengeneza network nyengine kwa matumizi ya baadae. Alibaki nyuma na mimi. Tuli enjoy, tuli jifunza na pia yeye aliweza kuweka MIZIZI yake vizuri ili mbuyu huu tunao uona leo usimame.
Mawe mengi mno kapigwa. Maneno mengi sana yamesemwa juu yake, kama binadamu hawezi kuwa amekamilika au kamaliza, ila jitihada zake na kazi ambayo anaifanya inabaki inamzungumza kwa niaba yake. Kama ambavyo yeye anasema, kwanza yeye ni MFANYA BIASHARA, mengine yanakuja baada ya hapo. Diamond anamlipa Sallam kwa asilimia kila mara anapoleta BIASHARA kwenye MEZA YAKE. Faida ni ya WOTE. Sio mmoja ananenepa na mwengine anakonda kama ilivyo kwenye mahusiano mengi ya biashara hapa nyumbani na pengine Afrika na duniani kwa ujumla.
Ukiniuliza mimi nitakuambia, hapa kuna mengi ya kujifunza.
Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahs...
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm
ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru
GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
Audiomack Link bit.ly/YahSton...
RUclips Link bit.ly/RUclipsS...
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz