Ombeni Stony - Na Wewe (Official Music Audio)

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 26 янв 2025
  • Kila kitu kwenye maisha ni safari, yani kina mwanzo na mwisho wake. Je, katika safari uliyonayo kwenye mahusiano, ndoa, elimu, biashara ama huduma yako!
    Una uhakika mwendo utaumaliza??
    .
    .
    Kwenye huu wimbo, nimeongea na Mungu kwamba "Nikiwa na wewe mwendo nitaumaliza, daima na wewe sina mashaka kamwe"
    Tunaweza waonea mashaka wanadamu lakini sio Mungu, Mungu wetu ni wa uhakika sana, anastahili kuanza na kumaliza nae katika mambo yetu yote. Na ndio maana Mussa alikataa kwenda na Malaika katika ile safari ya kutoka Misri kuelekea Kaanani, alimwamwambia Mungu "Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa", Yani aliona ni bora safari isiendelee kuliko kuendelea na Mungu asiwepo kwenye safari yao.
    Yote hii ni kwasababu alielewa hatari na hasara ya kuendelea na safari bila Mungu.
    Nikuombe wewe unayeanza biashara, huduma, Mahusiano, ndoa au masomo n.k usianze wala kuendelea peke yako, tuungane pamoja katika wimbo huu kukiri kwamba "Nikiwa na wewe mwendo nitaumaliza, daima na wewe mimi sina shaka kamwe" na Mungu ataanza kutembea na wewe kwa upya katika mambo yako.
    Nakutakia mafanikio mema katika safari yako ya maisha. Amen!!
    Kutoka 33:1-17 (Exodus 33:1-17)
    #OmbeniStony #Nawewe #Nikiwanawewe

Комментарии •