Askari Kukaa Kambini Miaka 6 Bila Kuoa / Kuolewa. Waziri wa Ulinzi na JKT, Atoa Ufafanuzi Bungeni

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 15 сен 2022
  • Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Stergomena Lawrence Tax (Mb) leo Septemba 16, 2022 ametoa ufafanuzi Bungeni kuhusu utaratibu uliowekwa kwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa kukaa miaka sita bila kuoa ama kuolewa mara baada ya kujiunga na jeshi hilo.
    Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax ameliambia Bunge kuwa kwa sasa utaratibu huo utabakia kama ulivyo kutokana na misingi iliyowekwa kwa ajili ya kuwaandaa askari hao kulinda nchi.
    Dkt. Stergomena amesema askari wapya wanaojiunga na Jeshi wanahesabiwa kama wapiganaji ambao wanapaswa kupewa ujuzi zaidi mara baada ya kutoka Chuo Cha Mafunzo ya awali (Recruit Training School) hivyo miaka sita iliyowekwa ya kutokuoa ama kuolewa inatoa nafasi kwa askari hao kutumika katika shughuli za medani pamoja na Oparesheni za Kijeshi kulingana na mahiiiijio.

Комментарии • 11

  • @mohamedfakili3376
    @mohamedfakili3376 Год назад +1

    Wanaorudishwa nyumba asilimia kubwa ni watoto wa wanyonge wasio na watu majeshini...

  • @boldleader94
    @boldleader94 Год назад +1

    Jeshi sio uraiani...km wanataka waone congo n.k , jeshi likiwa km taasis za kiraia,sio jeshi tutaharibu utendaji kazi...#Umoja

  • @mustaphawelder7022
    @mustaphawelder7022 Год назад

    Huyo wazir wa ulinzi mbona mrembo ataweza kweli kupambana na panya road

  • @shelyboyshely2928
    @shelyboyshely2928 Год назад

    Wacheni wakae miaka iyo Mbona wafungwa wanakaa miaka mingi bila wake bila waume au mnawachukuliaje awo wanaokaa mda mlefu msiwe mnapendelea sehem moja wote hao ni binadamu

  • @eraera2304
    @eraera2304 Год назад +1

    Hapo usawa uko wapi? punguzeni muda wa kukaa kikapera

  • @mburakhan978
    @mburakhan978 Год назад

    Umeongea

    • @telemlasamweli7262
      @telemlasamweli7262 Год назад

      Sawa kabisa lakini mnatakiwa kuwaonea huruma watoto wanao kuwa wamejitolea huko jkt na mkaamua kuwapa kipaumbele Cha ajira

  • @victorjames3730
    @victorjames3730 Год назад

    Ndio maana jeshini kuna HIV Kali Sana