🇹🇿 BASHUNGWA: SERIKALI YAPATA SULUHISHO LA MLIMA KITONGA

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 19 сен 2024
  • Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, amesema Serikali imesikia kilio cha Watumiaji wa barabara kuu ya TANZAM kutokea Ruaha Mbuyuni hususan eneo la Mlima Kitonga lenye urefu wa kilometa 7.6 na inakwenda kutoa suluhisho, ambapo tayari wataalam wamewasilisha mapendekezo ya muda mfupi na muda mrefu ambayo yatafanyiwa kazi na Serikali.
    Eneo hilo la Mlima Kitonga ambalo limekuwa kero kubwa kwa watumiaji wa barabara kutokana na kuwepo kwa mlima mkali na kusababisha foleni kwa muda mrefu pamoja na ajali za magari sasa Serikali inakwenda kuipanua kwa gharama ya Shilingi Bilioni 6.478 ikiwa ni makadirio ya utekelezaji wake katika mpango wa muda mfupi.
    Bashungwa amesema hayo mkoani Iringa wakati alipofika eneo hilo na kupata taarifa ya wataalam kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS) mara baada ya kukamilisha usanifu wa upanuzi wa Mlima Kitonga ili kuimarisha usalama kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Комментарии • 2

  • @godwinmwakibibi274
    @godwinmwakibibi274 11 месяцев назад

    Asanteni kwa hili maan watu Wa magari madogo+It tunakoma tukiovertake yaan ukae nyuma ya roli mpka mliman uishe kitu ambacho ni hatarii kwa usalama wetu so Nashukur mama Samia kwa kuamua hili ili ikiwezekana ujenzi uanze mara , moja#ilovemycountry

  • @khamiskiandiko2965
    @khamiskiandiko2965 11 месяцев назад

    Sijaelewa