Majaribio ya ndege uwanja mpya Dodoma kuanza Agosti

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 5 май 2024
  • Serikali imejiridhisha na kasi ya ujenzi ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa unaojengwa Msalato jijini Dodoma, ambao utagharimu kiasi cha zaidi ya Sh300 bilioni hadi kukamilika kwake.
    Hayo yamesemwa jana Mei 5, 2024 kwenye ziara ya Msemaji wa Serikali jijini Dodoma, ambayo ilikuwa na lengo la kukagua miradi ya kimkakati iliyoanzishwa na Serikali.
    Akizungumza na wanahabari, Msemaji wa Serikali Mobhare Matinyi, ameonyesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa Uwanja huo, ambao kwa awamu ya kwanza utafanyiwa majaribio ya kutua na kuruka kwa ndege ifikapo mwezi Agosti mwaka huu.
    Matinyi amesema kuwa matarajio ya Serikali baada ya uwanja huo kukamilika, ni kuwa utahudumia ndege za mashirika ya ndani na nje ya nchi.
    “Si tu kuhudumia ndege hizo ila pia Dodoma itaongeza idadi kubwa ya watu ambao watachangia ongezeko la uchumi wetu, hivyo wananchi na wenyeji wa Dodoma waanze kujiandaa kuchangamkia fursa hii,” amesema Matinyi.

Комментарии • 11

  • @erastuskajuna812
    @erastuskajuna812 18 дней назад +4

    Na uwanja uitwe Magufuli Airport kumuenzi muasisi wake

  • @ernestsinje9700
    @ernestsinje9700 Месяц назад +2

    Tanzania 🇹🇿 is developing fast

  • @ernestsinje9700
    @ernestsinje9700 Месяц назад +1

    Hongera serikali ya Tanzania

  • @leonardmrope9528
    @leonardmrope9528 Месяц назад +3

    R.I.p Rais Magufuli,,,

  • @mussamussa8181
    @mussamussa8181 Месяц назад +2

    Uyu wa pili na miwan yake nyeus chawa

  • @mussamussa8181
    @mussamussa8181 Месяц назад +1

    Nilicho penda uyo baba wa mwanzo sio chawa...kasema tu ukwel ilikuaga ndoto na awam ya 5 ikafanya ifanyike awam ya 6 inaendeleza saf kabsa

  • @jituakilimali15
    @jituakilimali15 Месяц назад

    Mnajenga vizuri lakini miundo mbinu Ya maji safi na maji taka hamna Takataka hamna namna Ya kuzichakata ni vitu muhimu sana katika ujenzi

  • @mussamussa8181
    @mussamussa8181 Месяц назад

    Unagalim sio utagalim

    • @berthatz
      @berthatz Месяц назад

      Utagharimu..jifunze kiswahili sanifu…

    • @salumalriyamy
      @salumalriyamy 13 часов назад

      Mtu hajui kuunda neno anataka kukosoa sentensi... Tanzania inazidi kupata vituko kila kukicha