Askofu Mwijage: Tusiogope kusema kweli daima/ Mafrater waweka kiapo cha Useja.

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 6 сен 2024
  • Wakristo wametakiwa kuwa waaminifu kwa kusema ukweli daima na kukemea mambo yasiyofaa katika jamii na kuwaonya wanaoenda kinyume na Mungu pamoja na kuwasihi Mafrater kushika njia ya Kristo bila kugeuka nyuma.
    Wito huo umtetolewa na Askofu Jovitus Mwijage, Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba wakati wa homilia yake katika adhimisho la Misa takatifu ya kuweka Kiapo cha Useja kwa Mafrater watano Kabla ya Misa ya Ushemasi Jimboni Bukoba.
    Katika homilia yake Askofu Mwijage amesema kuwa Mungu ndiye pekee mwenye haki,
    Kwa mfano wa wayahudi walimuua Kristo kwa kutofumbia ukweli kwa dhuluma walizozifanya vivyohivyo waamini wanatakiwa kusimama kidete na kukemea maovu yanayotendeka katika jamii inayyotuzunguka.
    Aidha Askofu Mwijage amesema kuwa Jamii ya sasa haipendi wanaozungumza ukweli kwani kwa kuwa na malengo yanayoingilia maslahi yao, na kuongeza kwa kusema kuwa msema kweli atazushiwa na kuchafuliwa jina lake kama ilivyokuwa kwa Yesu Kristo mwenyewe na kuendelea kuwasihi Mafreater walioweka kiapo hicho kuwa imara kwa kufuata njia ya Kristo bila kurudi nyuma na kutakiwa kutembea kifu mbele wakitambua kuwa wanamtagza Kristo.
    Mafrater walioweka kiapo cha Useja Jimboni Bukoba kabla ya Misa takatifu ya Ushemasi ni Frater Allanus Kabobo wa Parokia (Kishogo), Frater Beatus Kaijage Parokia Kagondo, Frater ⁠Cassius Rwelamiza Parokia Ngote, Frater Prudence Mujwahuzi Parokia Minziro na Frater Willbrord Ndyamukama Parokia ya Itahwa, wote wanatarajiwa kupatiwa Daraja ya Ushemasi kesho Marchi 16 2024.
    www.radiombiu.co.tz
    #RmSautiYaFaraja

Комментарии • 1

  • @user-qn9ip4bx2y
    @user-qn9ip4bx2y 5 месяцев назад

    Mwenyezi mungu naomba atujalie amani na upendo apa duniani na uko mbinguni tusitaili kuufikia ukamilifu na uzima wa milele amina