Mwanamke Bomba | Caroline Menach anatoa mafunzo kwa wanawake

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 10 фев 2025
  • Mila na desturi za jamii ya Wapokot kwa miaka mingi hazijamruhusu mwanamke kushiriki kikamilifu katika masuala ya kiuchumi. Hata hivyo, hali sasa imeanza kubadilika kutokana na juhudi za wadau mbalimbali akiwemo Shujaa Caroline Menach. Licha ya kuwa mwalimu, Caroline amejitwika jukumu la kuwaelimisha wanawake kuhusu umuhimu wa kilimo ili kujipatia mapato. Kupitia juhudi zake, wanawake wa eneo hilo kame wameanza kujihusisha na shughuli za kilimo, jambo ambalo limewapa uhuru wa kiuchumi na kuwasaidia wanaume wao kuongeza mapato ya familia.Caroline ambaye alitunukiwa tuzo ya Hsc mwaka 2021 na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta ndiye anayetupambia makala yetu ya mwanamke bomba hii leo.

Комментарии • 2