Kaburi Tupu: Ushuhuda wa Kaburi la Yesu || Somo 12 | 18/ 12/ 2024

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 3 янв 2025
  • Soma Yohana 20:1-7. Kuna umuhimu gani kwetu kuhusu kile kinachoelezewa katika aya hizi?
    Yesu alikufa Ijumaa alasiri na alifufuka alfajiri na mapema Jumapili. Kwa sababu Sabato ilikuwa imekaribia alipozikwa (Yn. 19:42), mchakato wa maziko ulifanyika kwa haraka na haukukamilika. Ingawa walimpenda Yesu sana, wafuasi Wake waliitunza siku ya Sabato na hawakwenda kaburini (linganisha na Mk. 16:1, Luka 23:56). Baada ya Sabato, wanawake kadhaa walinunua manukato ili Kuja nayo kaburini Jumapili asubuhi. Kwa mshtuko wao, jiwe lilikuwa limeondolewa, na kaburi lilikuwa tupu.
    Mariamu Magdalene alikuwa mmoja wa wale waliofika kaburini mapema. Alikimbia kwenda kuwaambia Petro na Yohana kile alichokiona. Watu hao wawili walikimbia kwenda huko. Yohana alimzidi mbio Petro na kufika wa kwanza. Akainama chini, akachungulia ndani, akaona sanda ambayo Yesu alikuwa amefungwa. Lakini hakuingia ndani.
    Hata hivyo, Petro aliingia ndani na akaona sanda ikiwa imelazwa humo. Pia, aliona leso ambayo iliyokuwa kichwani pa Yesu, lakini haikuwa pamoja na vitambaa vingine. Ilikuwa imekunjwa na kuwekwa kando.
    Soma Yohana 20:8-10. Nini maana ya leso iliyokuwa imekunjwa?
    Baada ya Petro kuingia kaburini, ndipo Yohana naye akaingia. Yohana 20:8 inasema kwamba aliingia, akaona na kuamini. Kwa nini kuona vitambaa vya sanda vimelala pale na leso ikiwa kando, ikiwa imekunjwa, kungemfanya Yohana aamini kwamba Yesu amefufuka katika wafu?
    Ili kujibu swali hili, ni muhimu kutafakari kwa nini kaburi lilikuwa tupu kwa kuanzia. Jibu la kawaida zaidi lingekuwa wizi kaburini. Lakini maelezo haya si ya kweli kwa sababu tatu, Kwanza, Mathayo anatwambia kwamba kaburi lililindwa ( Mt. 27:62-66 ), na kufanya wizi kaburini usiwezekane. Pili, wezi wa makaburini kwa kawaida huiba vitu vya thamani, si miili inayooza. Tatu, wezi wa makaburini wako katika haraka na hawakunji vitambaa vya sanda. Si ajabu, basi, kwamba Yohana alipoiona leso iliyofungwa kichwani kimekunjwa, aliamini kwamba Yesu alikuwa amefufuka ufuni.

Комментарии •