Kuna Aina Mbili za Macho

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 26 сен 2024
  • Yesu Kristo katika mojawapo ya mafundisho yake, alitoa kipaumbele sana kuzungumzia juu ya aina hizi mbili za macho. Mathayo. 6: 22 - 23 ;
    Luka. 11 : 34 - 36.
    *Alizungumzia juu ya macho haya ya nyama ambavo kila mmoja wetu anafahamu
    umuhimu wake; yaani macho haya ya mwili, Yesu akasema wazi kwamba macho haya ya mwili yakiwa safi (mazima), mwili wako wote unakuwa na NURU, bali macho yako yakiwa mabovu; mwili wako wote unakuwa GIZA!!! alimaanisha wazi kwamba maendeleo yote ya mwili huu, furaha yote ya mwili huu kama kupata elimu nzuri, kufurahia kazi nzuri, nyumba nzuri, gari zuri, mke mzuri, mume mzuri n.k. kunahitaji macho haya ya mwili yawe mazima kwanza; ndiyo maana binadamu wanalinda na kutunza macho yao ya mwili sana; na ukiwa kipofu tu, unaishi kwa kutegemea msaada wa mtu mwingine hata kama una elimu, ni tajiri, umeoa/ umeolewa, lazima unaanza kutegemea mtu mwingine akuongoze. Kweli taa ya mwili ni jicho linaloona.
    2. Kazi ya macho haya ya mwili _ hasa ni MBILI tu.
    a.) KUONA kitu kizuri na kuleta taarifa kwa ndugu moyo kwamba kitu hiki ni kizuri na kinakufaa, na moyo unapeleka taarifa kwa ndugu mwili ili afanye juu chini ili akipate.
    2 Samweli. 11 : 3 - 5, Mwanzo. 3 : 5 - 6
    ( tamaa zote za mwili nzuri na mbaya zinaongozwa na macho ) ; Macho ndiyo yanayoona fursa kwanza hata kama ni za madini, biashara n.k. Yana uwezo mkubwa wa kufanya ufanikiwe kimwili na kiroho; lakini pia yana uwezo mkubwa kukuangusha sana na kukukosesha.
    Mathayo. 5 : 27 - 29, Marko. 9 : 47 - 48
    b. Kuona HATARI na kuleta taarifa kwa ndugu moyo ambaye anapeleka taarifa kwa ndugu mwili ili achukue taratibu za kupambana au kukimbia, au kupiga yowe n.k.
    2 Wafalme. 6 : 15, Kutoka.14 : 10 - 12,
    1 Samweli 17 : 4 - 11, 32 - 33. 1 Samweli. 17 : 41 - 44.
    ( Macho ndiyo yanayoona vitisho vyote vya maisha haya kwanza, na yakitishika
    yenyewe ( yakiogopa ) , taarifa hii inasambaa mwili mzima na huwezi kufanya jambo lolote la kijasiri kamwe.)
    Macho haya ya mwili kazi yake muhimu na kuu sana ni kutoa taarifa kwa ndugu moyo kwamba hapa tumekwisha, na moyo unatoa taarifa kwa ndugu mwili kwamba tafuta namna yoyote ya kujiokoa/kujitetea/kujificha.

Комментарии • 1

  • @yusuphlean417
    @yusuphlean417 5 месяцев назад +1

    Nakushukuru MUNGU kwa kunipa macho mazuri na yenye nuru. BARIKIWA SANA MTUMISHI WA MUNGU