Jux: "Show Yangu Ya Kwanza Nilikuwa Na Diamond, Nilipewa Elfu Hamsini" | SALAMA NA JUX PART I

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 12 дек 2024
  • #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
    Juma Jux ni mtanashati haswa hicho ndicho cha kwanza na suala la yeye pia kuwa muimbaji mzuri (na anayeendelea kujengeka) kunamfanya pia awe wa kipekee, anajua maana halisi ya kufanya kazi kwa bidii ili uweze kutimiza malengo ambayo wewe unakua umejiwekea. Ana aibu pia sana ila hili unaweza ukalitilia shaka kwasababu ya kazi aliyoamua kuichagua. Kwa nilivyo muelewa mimi yeye aliamua kufanya muziki kwasababu rafiki zake walikua wanafanya muziki na zaidi akiamini yeye ni Rapper kuliko hata kuwa muimbaji.
    Kwa mujibu wake kwenye kundi lao hilo la shule yeye ndo alikua sio mkali na wala hakua na neno juu ya hilo, zaidi yeye alikua anataka ku fit in zaidi. Lakini leo hii yeye ndo mwenye mafaniko zaidi kwenye fani yake kuliko wale walokua ndo wakali wa kazi hizo wakati bado wako shuleni. Jux ananiambia mpaka leo wanaendelea kuwa marafiki na rafiki zake wa shule, zaidi Cyrill Kamikaze ambaye amekua kama ndugu yake. Pia anakumbuka mara ya kwanza wimbo wake ulipoenda redioni bila ya matarajio yake na wakati anaambia B12 ameupenda na angependa akutane nae anasema baridi na uwoga na aibu aliyokua anasikia ni Mungu pekee ndo anajua.
    Uzuri pia Jux ana muonekano mzuri na utanashati wake umekua ukimfanya ajikusanyie mashabiki wengi haswa wanawake na ku inspire vijana wengi watake kupita kwenye nyendo zake ili nao waweze kuja kuwa kama yeye siku moja. Combination yake na Bob Maneke nayo ni kitu ambacho kimemfanya Jux aendelee kuwa pale. Wanafahamiana vizuri na kazi ambayo wamekua wakiifanya pamoja imekua ikijieleza yenyewe.
    Jux anakumbuka utanashati na kujituma kwa Marehemu Baba yake ambaye kwa maelezo yake anasema alikua Baba BORA sana, kwanza hakuwahi hata siku moja kumuona Mzee wake na Mama yake wanagombana na siku zote alikua anahakikisha watoto wake wanaishi na kusoma vizuri, nadhani nia yake ilikua kutaka kuwaona watoto wake wakiwa wasomi labda na kufanya kazi za maana zaidi au kuishi maisha mazuri zaidi kuliko yeye wakati anakua. Jux ana kumbuka Mzee wake kama mtu wa kujituma sana ambaye alijichanga kumfikisha mkewe mjini baada ya kupata kazi, yeye alikua tu fundi wa magari ila baada ya mke wake kupata kazi mjini, alihakikisha anafika na mambo mengine yaende kwa uzuri kama ambavyo alikua akiyataka kwa wanawe.
    Mama yake pia humuambia zaidi siku hizi za karibuni baada ya Jux kuanza kung’ara kwenye muziki na biashara zake, Mama yake anamuambia anamkumbusha mno Marehemu mume wake na anajua fika kama angekua hai basi angekua anajivunia yeye kupita kiasi. Uvaaji wake na utanashati na jinsi ambavyo anajituma hivyo vyote Juma Jux amerithi kutoka kwa Marehemu Mzee wake. Mwenyezi Mungu Aendelee Kumpumzisha kwa Amani.
    Mapenzi yake ya dhati ambayo huyaonyesha kwa watu ambao amekua nao katika mahusiano nae pia kwa kiasi kikubwa amechukua kutoka kwa wazazi wake, jinsi ambavyo Baba yake alivyokua anampenda Mama yake, ni kitu ambacho Juma amekua akikikubali sana. Na yoyote ambaye anakua nae amekua akifanya analoweza ili waendelee kudumu. Mwenzetu amekua na mwalimu mzuri sana.
    Kwa akili ya muziki na biashara nadhani tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa kijana huyu hodari wa ki Tanzania. Hivi karibuni brand yake ya African Boy imetia makubaliano na kampuni moja kutoka China ambayo wamekua wakimuona Juma anafanya biashara hiyo tokea akiwa mwanafunzi na kwa jinsi ambayo amekua akifanya kwa muda mrefu na brand na yeye kama mwanamuziki kuzidi kukua nadhani na wao pia waliona fursa ya kufanya nae ushirikiano ili waweze kumuwezesha zaidi ili waweze kushinda WOTE.
    Yangu matumaini kama ada uta enjoy episode hii na kujifunza zaidi.
    Love,
    Salama.
    Support us through anchor.fm/yahs...
    SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
    Listen our Podcast on
    Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
    ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
    GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
    Audiomack Link bit.ly/YahSton...
    ‪RUclips Link bit.ly/RUclipsS...
    Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
    Follow:
    Twitter: / yahstonetown
    Instagram: / yahstonetown
    Facebook: / yahstonetown
    Channel Administered by Slide Digital
    Instagram: slidedigitaltz

Комментарии • 83

  • @noelbernard6390
    @noelbernard6390 2 года назад +5

    Salama naomba umlete masoud masoud, yule Mzee ana vitu vikubwa Sana.

  • @ilhamsalum6815
    @ilhamsalum6815 2 года назад +5

    Hiki kipindi kishajaza dayari yng salama, thanks so much najifunz mengi 💞

  • @tantinebettynduwimana380
    @tantinebettynduwimana380 2 года назад +4

    Salama umependeza ulipo jistiri mashallah

  • @sankybadee7894
    @sankybadee7894 2 года назад +2

    Salama my sister umekua bibi now Sasa duh bigup sana

  • @fralex_1276
    @fralex_1276 2 года назад +1

    Nice sema jux mdomo kapaka sukari itakuwa maan sio kwa kuulamba huko

  • @fredyjuma1121
    @fredyjuma1121 2 года назад +3

    Shangazi Fanya bdozen afike Apo ! 🏌️‍♂️ 🔥🔥🔥

  • @uzungupoint
    @uzungupoint 2 года назад +2

    You're so cute Salama, narudia kuangalia tabasamu lako muda wote najikuta nasmile mwenyewe jamani ♥️😊

  • @barnabasmafuru6735
    @barnabasmafuru6735 2 года назад +1

    Dada Salama unajuaa sanaa na unanifundisha kufanya jambo kwa ufanisi na ufasaha wahari ya juu maana kufanya tuu haitoshi kila mtu anaeza fanya.

  • @thebeneficialknowledge3399
    @thebeneficialknowledge3399 2 года назад +4

    Kudos to you and your whole team “Salama” you are indeed amazing at what you do, tunasoma mengi kupitia interviews zako, keep up the good work my Zanzibari sis… love from the UK.

  • @sweetie6934
    @sweetie6934 2 года назад +7

    Iko wapi interview ya binti Zuhura Othman Soud @ Salama

  • @chillahthomas3265
    @chillahthomas3265 2 года назад +17

    Salama is Africa's Ellen Degeneres

  • @flavianchuwa4370
    @flavianchuwa4370 2 года назад

    Kipindi Bora Sana Asante Salama Allah azidi kukulinda

  • @danielafelix9856
    @danielafelix9856 2 года назад +3

    I’ve Never missed an episode 🙈😍

  • @wairimu9113
    @wairimu9113 2 года назад +3

    jux is a fine man,God did take his time on him😍😍

  • @salimbazmul5806
    @salimbazmul5806 2 года назад +5

    Big Up Sis Salama....✊Shabiki Sugu Huajawahi nifelisha

  • @nasmasalimu9508
    @nasmasalimu9508 2 года назад +3

    Wow big up sis love you 😍

  • @saidabdulkadirmjahid8255
    @saidabdulkadirmjahid8255 2 года назад +3

    Chemistry ya #Manecky and #jux is always 🔥🔥🔥

  • @ramakadege7448
    @ramakadege7448 2 года назад +2

    Big up salama j

  • @liciouscharles3370
    @liciouscharles3370 2 года назад +5

    Cyril kamikaze is a GEM

  • @emojimakopakopa
    @emojimakopakopa 7 месяцев назад

    Bro nakubali sana

  • @lastsimbatv1497
    @lastsimbatv1497 2 года назад +2

    Cjawah miss hta kdg salam nakukubar san mlete mondi

  • @ibbu-tz
    @ibbu-tz 2 года назад +2

    Ramba ramba lips sana mzee 🥲🥲🥲

  • @HurumaMwaseba
    @HurumaMwaseba 4 месяца назад

    Naangalia hapa

  • @mwajumabinwa604
    @mwajumabinwa604 2 года назад +1

    your mom she is here or she’s alive 😁🥰🥰🥰

  • @zejuchaztips353
    @zejuchaztips353 2 года назад +2

    Jux is the best

  • @papaamayux-paps7883
    @papaamayux-paps7883 2 года назад +1

    mbona hii interview haipo Podcast

  • @richardcastromzena5136
    @richardcastromzena5136 2 года назад +1

    6:13Kujiskia studio mara ya kwanza ni magical
    17:40

  • @edwardmachaku1661
    @edwardmachaku1661 2 года назад +1

    Salama, Congratulations 🎉

  • @leejames1536
    @leejames1536 2 года назад +1

    my mom she's proud of me✋😂...sawa kaka

  • @deograsiaomary62
    @deograsiaomary62 2 года назад

    Salama mbona interview zako nyingi unavaa nguo nyeusi

  • @BBrown_vevo
    @BBrown_vevo 2 года назад +1

    Big interview

  • @issrahayattv1356
    @issrahayattv1356 2 года назад +2

    Kama we ni fun w hipop tujuane hapa 😆 salama atami hua nasikiliza aren b ila c vile sana bt jux namtambua nimnyamwezi sn, please pitieni kw Chanel yngu pia kuna mazuri

  • @gsmartcreation5655
    @gsmartcreation5655 2 года назад +1

    Salama Aliwahi kumsaidia Godzilla Katika kuhakikisha anatumia “La na Ra” kwa usahihi. Hili swala hata kaka yetu Juma linamsumbua. Je, kuna msaada wowote anaweza pata hata akiwa studio? Maana inakuta anaimba vizuri Ila unasikia “Nipo Sarama ….” Msaada please

    • @josephstephen1079
      @josephstephen1079 2 года назад

      Hiyo inategemea na asili ya mtu pia mahali alipokulia

  • @salumpagae1757
    @salumpagae1757 2 года назад +2

    Misosi akuna😆😆

  • @MARTIN_M9.
    @MARTIN_M9. 2 года назад +2

    hii mbona kama imerudiwa🙄

  • @witnaofficial
    @witnaofficial 5 месяцев назад

    Naweza tumika Na jux pia,nikipata bahati

  • @khamisimtame7848
    @khamisimtame7848 2 года назад +1

    🔥🔥

  • @daudisaidi2267
    @daudisaidi2267 2 года назад

    🚀🚀

  • @samwelisaid5013
    @samwelisaid5013 2 года назад +1

    👍👍👍

  • @__thereal_unclechibo_7953
    @__thereal_unclechibo_7953 2 года назад

    Msanii gn unaitwa juma😂😂😂😂😂

  • @nicksonchesco233
    @nicksonchesco233 2 года назад +2

    Hii ndio nilikuwa naisubir

  • @vincentmchau5903
    @vincentmchau5903 2 года назад +2

    Salama kwann usiwe na watazamaji live ?

  • @officialaftab8760
    @officialaftab8760 2 года назад +1

    GOOD JOB ...,

  • @queenmaa30
    @queenmaa30 2 года назад +3

    My mom she's proud of me....jomon kidhungu....

  • @adamjoseph9370
    @adamjoseph9370 2 года назад +1

    #AsohiliAnaLile

  • @lizaeli6732
    @lizaeli6732 2 года назад +2

    Jamani mtuletee Vicent Kigosi

  • @khadijamisayo7476
    @khadijamisayo7476 2 года назад +1

    mwanamuziki ninae mpenda

  • @abdulraufmohammedsalum6806
    @abdulraufmohammedsalum6806 2 года назад +1

    Wakishua hawatumii nguvu nyingi kutoka

  • @abdallahkhamis7663
    @abdallahkhamis7663 2 года назад +1

    Show huwa inarushwa chanel gani, siku na muda gani pia tafadhali kwa anayefahamu naomba msaada?

  • @mshangaf1726
    @mshangaf1726 2 года назад +1

    kwa hiyo yale majina flani ya vinywaji vya hapo huwa kuna baadhi ya watu huwaambii ???😁😁😁

  • @TradersEasyWay
    @TradersEasyWay 2 года назад +3

    salama umenichekesha, eti ulishwai kuiba? ili swali limekea la ghafla..hahaha

  • @ommietrendz7175
    @ommietrendz7175 2 года назад +2

    Jux kutoka google unamiaka 32/33 12 yrs ago ulikuwa 20/21 sio 13/14 bro 😎

  • @johannahakim8470
    @johannahakim8470 2 года назад +3

    Sasa iyo midomo inakuwasha bro,ata miye nakupendaga mpaka Na nyimbo zako, Ila sipendagi mukiwaga mu ma Interview mukivala izo ma RAYBAN yani Ama mko bipofu mjikeribishi,acha nikamtizama kipenzi changu DIMPOZ

  • @Memphisblue22822
    @Memphisblue22822 2 года назад +2

    Kwamba diamond yup out of reach au?

  • @Soft_Touch7
    @Soft_Touch7 2 года назад +1

    @salama hii interview Na Jux ni ile ile tu mlofanya nae kwny MKASI…badilika kidogo dada no hard feelings

  • @ziyandamhlana8776
    @ziyandamhlana8776 2 года назад +4

    Sorry awant knw sister Salama long time people iknw why you don’t bring your husband to do interview

    • @Ibra_Canaan
      @Ibra_Canaan 2 года назад +3

      Bro hiki ni kingereza au?

    • @bekatiptop8910
      @bekatiptop8910 2 года назад +4

      First go and interview your English😂

    • @SalamaAJabir
      @SalamaAJabir 2 года назад +1

      Mi I wait fo your husband fast

    • @manfredmanda5388
      @manfredmanda5388 2 года назад +1

      @@SalamaAJabir 😅😅😅😅

  • @kelvinduper
    @kelvinduper 2 года назад +2

    Daradara😤

  • @anwaralimuhammed1481
    @anwaralimuhammed1481 2 года назад

    Tunaitaji aje tena king Kiba

  • @masungajonath8339
    @masungajonath8339 2 года назад

    AFB

  • @nasralema749
    @nasralema749 2 года назад

    Ankal katoweka

  • @ziyandamhlana8776
    @ziyandamhlana8776 2 года назад +1

    Onasasa unakuta jama sio tena mtuu wako

    • @omarymhomakilo7215
      @omarymhomakilo7215 2 года назад

      Maisha yanatakiwa kuendelea unatakiwa kuwaheshimu tu hata Kama hampo pamoja

  • @noelbernard6390
    @noelbernard6390 2 года назад

    Salama naomba umlete masoud masoud, yule Mzee ana vitu vikubwa Sana.